SoC02 Lima matunda uinuke kiuchumi na boresha afya yako

SoC02 Lima matunda uinuke kiuchumi na boresha afya yako

Stories of Change - 2022 Competition

Asantesanasana

New Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3
Reaction score
2
Napenda kutoa ushauri kwa kila mtu anayeweza kupanda miti ya matunda ya aina mbalimbali apande kwa wingi,ikishindikana kupanda kwa wingi, panda angalau hata miti mitatu ya matunda aina tofauti tofauti kwani kuna matunda yanatofautiana misimu japo matunda mengi yanafanana misimu ya upatikanaji wake na aina nyingine yanapatikana muda wote.

Kutokana na kupanda matunda tutapata pesa ambayo ni endelevu kwani miti mingi ya matunda ni ya muda mrefu na umri wa mti wa matunda unavyoongezeka na wingi wa mavuno unavyoongezeka ,kwa hiyo hata pato lako litaongezeka.

Pia huhitaji kuwa na mtaji au fedha nyingi sana kuwekeza kwenye kilimo cha matunda kama una ardhi hata kama una eneo dogo,unaweza kuanza na miti michache.

Napenda nitolee mfano wa mparachichi.Nilijifunza kutoka kwa jirani ambaye aliona fursa ya kupanda miti ya parachichi,wakati anaipanda tuliona kama hamna umhimu na anapoteza muda.

Alipoanza kuvuna matunda na kuuza tulishangaa pesa aliyoipata kutoka kwenye miti kumi tu ya parachichi.Kila mti uliweza kumpa zaidi ya shilingi laki moja ,ndipo tukajua kuwa miti ya matunda ni mali.

Matunda hayawezi kukosa soko,soko la kwanza ni nyumbani kwako,unakula wewe pamoja na familia yako kwa ajili ya kuboresha Afya zenu,usipo panda matunda utalazimika kutumia pesa kwenda kununua matunda,ambapo pesa hiyo ingetumika kwa shughuli nyingine.

Pia wanunuzi wa matunda kwaajili ya biashara ni wengi sana ,kwa hiyo uhakika wa kupata pesa kama wewe ni mkulima wa matunda ni mkubwa na niendelevu.

Pia kuna matunda kama parachichi yanaweza kuwa chakula cha mifugo mbalimbali,hivyo kupunguza gharama za chakula cha mifugo.

Pia unaweza kujitengenezea mafuta ya kula au kupaka mwilini kutoka kwenye tunda la parachichi. Unaweza kutumia majani au mbegu ya ndani ya parachichi kama dawa.

Kiujumla kilimo cha matunda kina faida lukuki.

Ushauri wangu, nakushauri panda miti ya matunda ,kwani utapata pesa endelevu,utaboresha Afya yako na pia utalinda mazingira.

Mimi nimeanza nawe anza sasa.

Asante.

Namba yangu ya simu_0710425986
 
Upvote 2
Back
Top Bottom