Limbwata la Florence Harding

Limbwata la Florence Harding

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2013
Posts
735
Reaction score
1,467
LIMBWATA LA "FLORENCE HARDING", LILIMFANYA BWEGE RAIS WA NCHI, AKASHIKWA AKASHIKIKA KISHA AKAUWAWA.

Na Comred Mbwana Allyamtu.
Wednsday - 10/7/2019
Dumila, Kilosa DC, Morogoro - Tanzania

Huku Afrika "Limbwata" ni dawa za kimazingara ambazo inadaiwa mwanaume akilishwa anakuwa zoba, kwa hiyo baada ya hapo mke anaweza kufanya anavyotaka na mume asiwe na kauli. Mwanaume wa hivyo mara nyingi huitwa bwege, yaani mwanaume aliyezubaa na anayetia aibu kwa wanaume wenzake juu ya vitimbwi vya mkewe anavyoshindwa kuvidhibiti, Lakini kileo kuna Limbwata za kidigitali yani mke anaku pagawisha na mahuba ya ukweli, ukichamganyikiwa tu imekula kwako, utaendeshwa mpaka utaomba pooo!!

Limbwata bwana haina hadabu, aitazami mamlaka au madaraka humuadabisha yoyote hata kama ni mfalme wa nchi au kiongozi machachari, nazani mzee Mugabe anajua kuhusu msamiati huu, kwani mmesahau habari za Luti na mkewe, au kisa cha Ngoswe? Hiyo tisa kumi ni kwamba hii Limbwata bwana ilimpeleka puta rais wa 29 wa Marekani, Warren Harding naye alikuwa mnyonge kwa mkewe, hakuwa mnyonge bure bure, ilikuwa limbwata bwana! Nazani sasa unanielewa.. Ehhh ndio mke wa prezda huko Marekani wakati huo Florence Harding alimwendesha kweli kweli mmewe wakati huo, mpaka magazeti yaliandika kuwa nchi ilikuwa inaongozwa na First Lady.

Unajua huyu mke wa Warren Harding alianzia wapi kumkamata mmewe? OK ili kuwa hivi, kwanza mwaka 1919, taifa la Marekani lilikuwa linaingia kwenye uchaguzi mkuu wa kumtafuta rais wa 29, hivyo Warren Harding nae alitangaza kuwania Urais wa Marekani. Kutokana na ushawishi wake kuwa mdogo akaonekana msindikizaji kwakuwa hakuwa amejiandaa kisiasa, unajua katika historia Warren Harding ni mmoja ya watu wenye bahati sana ehh! Ndio! maana yeye ni moja ya watu walio okota mdodo chini ya mkaratusi, ebu twende sawa utanielewa mbeleni kwanini niseme aliokota mdodo chini ya mkaratusi! ilikuwa hivi, Kulikuwa na wanasiasa wenye nguvu ndani ya Republican kumzidi yeye kwa mbali sana, mchakato wa kura za uteuzi wa chama ulipoanza, Harding alichakazwa vibaya.

Baada ya kuona ndoto yake inafifia kufatia kipigo katika mzunguko wa kwanza ndani ya chama ambapo Harding alipoona nafasi nne za juu hayumo, alikata tamaa. Akampigia simu meneja kampeni wake aliyeitwa Harry Daugherty, akamwambia anajitoa. Mke wa Harding aliyeitwa Florence, aliposikia mazungumzo ya mumewe na Daugherty, alikata simu. Akamwambia hakuna kujitoa mpaka mkutano mkuu upite, punda afe lakini mzingo ufike.

Mwana mama Florence akamuona mmewe dhaifu, akaapa kusimamia mziki mwenyewe, wakati huo bado mme wake alisisitiza kujitoa, japo hilo mke wake alilipinga sana ndipo Florence alimwambia Harding kuwa "mwanaume si mkata tamaa ni mpambanaji", maneno haya yalimpa nguvu sana Harding akaelewa somo, kisha akamjibu kwa kusema "Well, you tell Harry Daugherty for me that we're in this fight until Hell freezes over" yani "Vizuri, mwambie Harry Daugherty kwa niaba yangu kwamba, tupo kwenye hili pambano mpaka Jehanamu ifunikwe na barafu".

Siku ya siku mkutano mkuu ukawadia, lakini Mungu alivyo mkuu ikaibuka kashfa ya matumizi makubwa ya fedha bwana, waliokuwa wanaongoza mbio za uteuzi, yani Jenerali Leonard Wood, aliyekuwa Gavana wa Illinois, Frank Lowden, Seneta wa California, Hiram Johnson na Rais wa baadaye wa nchi hiyo, Herbert Hoover, walionekana wametumia pesa nyingi na wangeweza kukigawa chama cha republican hivyo Juni 11, 1920, kura za mkutano mkuu zilipigwa, hakuna aliyefikisha kura 498 zilizohitajika ili atangazwe mgombea rasmi kwa mujibu wa kanuni za chama hicho, kwani Wood alipata 314, Lowden 289, Harding aliambulia 65 lohhh! Mungu akitaka kukuibua kuwa David atakushusha kwanza, Usiku wa siku hiyo, wazee wa chama (Super delegates power) waliwaomba wajumbe kumchagua Harding ili kukinusuru chama, baada ya mivutano mwisho Warren Harding akapitishwa kugombea urais kisha akachaguliwa kuwa Rais wa 29 wa Marekani, hii ndio Mungu akipanga hakuna wa kupangua na ile mdodo chini ya mkaratusi ikakamikika.

Kwakuwa Florence, yeye ndio alipambana mpaka mumewe kushinda akavimba kichwa, akawa yeye ndio Maraekani, alisisitiza kumwambia mme wake kuwa bila yeye wala Warren Harding asingekuwa rais wala kuikanyaga White House, hivyo akaanza kumdhibiti mmewe, aliagiza intelijensia kufanya kazi kudhibiti wote asio wapenda, alimwandikia Rais Harding cha kuzungumza kwa waandishi wa habari, Florence akuishia hapo kwani yeye ndiye alikuwa kila kitu kwa Serikali ya Marekani, ilifika hatua Florence aliwahi kusema yeye ndiye sauti ya Rais, ebwane we! Usichezee Limbwata, sijui alimpa nini mzee wa watu.

Maana yeye alimkamata sawa sawa mzee wa nchi, hakuna kilicho fanyika bila ridhaa yake hata kama ni swala lilo husu nchi, loh! Huyu alikuwa kiboko, nchi yote ilimuheshimu Florence Mabel Harding, mke wa rais, ilifika mahali hata watumishi wa nchi walimuogopa Florence kuliko raisi mwenywe, huyu kweli alikuwa jiwe sio kama hawa wakina Hillary Rodham Clinton ambaye alikuwa mke wa Rais wa 42 wa taifa hilo, Bill Clinton au mke wa Rais wa 32, Franklin Roosevelt, aliye itwa Eleanor, au Abigail Adams, ambaye ni mke wa Rais wa Pili wa Marekani, John Adams, ambae pia ni mama wa Rais wa Sita wa nchi hiyo, John Quincy Adams, au Jacqueline Kennedy, mke wa Rais wa 35, John F. Kennedy, au Claudia Alta Johnson ‘Lady Bird Johnson’, mke wa Rais wa 36, Lyndon Johnson au mama la mahaba Michelle Obama.

Huyu Florence Harding ndiye mke wa Rais wa Marekani, aliyeitikisa Ikulu ya nchi hiyo, White House kuliko wengine wote. Zaidi inaaminika ndiye First Lady aliyekuwa na akili nyingi kupita wote walio mtangulia na walio mfuata mpaka leo, kwani Florence aliitumia White House kutimiza matakwa yake kuliko hata mume wake, Warren Gamaliel Harding, kwani Rais Harding alizidiwa akili na Florence kwa mambo mengi sana, kwanza zipo hotuba nyingi ziliandikwa na mkewe ikiwemo ile ya kuapishwa kuwa rais aliyoitoa Machi 4, 1921, ilielezwa kuwa ziliandikwa na Florence. Vyombo vya habari Marekani, viliamini kuwa Florence alikuwa na uwezo mkubwa wa kuandika hotuba zenye ushawishi kuliko Rais Harding.

Ni kwa sababu hiyo, Florence alikuwa na ushawishi mkubwa na upo uamuzi ambao ulifanywa na Rais Harding lakini vyombo vya habari na wapinzani wa kiongozi huyo, walibeza kwa maelezo kuwa ni maagizo ya First Lady (Florence). Katika mazingira hayo, Rais Harding alishambuliwa kuwa alikuwa akipelekwa puta na Florence akikosa namna ya kujipambanua kuwa yeye ndiye mume na ndiye Rais, kwamba mke wake alikuwa na msuli mkubwa kuliko mume.

Huyu Florence unaweza kumwita First Lady wa Ma-First Lady bwana hakuwa wa mchezo, maana ni wa kwanza kwa kila kitu, alikuwa mke wa kwanza wa Rais wa Marekani, kuandaa sherehe za mara kwa mara White House, alialika watu kwa chakula cha jioni na kuwaburudisha kwa kutazama filamu baada ya chakula, alikuwa na utaratibu wa kualika mcheza filamu mkubwa Ikulu na kula naye chakula, iwe cha mchana au jioni, alifanya hivyo alivyojisikia na Rais Harding hakuwa na ubavu wa kupingana na hilo, hata akuweza kukemea maana alikuwa First Lady wa kwanza kucheza filamu mume wake akiwa Rais! Unashangazwa na hili? usishangae ndio alicheza filamu katika kipande cha utangazaji wa taarifa ya habari, alifanya hivyo kwa sababu alipenda sana taaluma ya uandishi wa habari, ingawa sheria za nchi hiyo kipindi hicho azikuruhusu lakini nani angeweza kuthubutu kumzuia?.

Florence alikuwa na tabia ya kujibu barua za Rais na kutoa maelekezo bila mume wake kujua, baada ya kufanya hivyo, alimjulisha mume wake kuhusu uamuzi ambao aliufanya kwa niaba yake kupitia barua zenye nembo na mhuri wa Rais wa Marekani, alikuwa akiandaa sherehe (party) mara kwa mara ndani ya boti la Rais wa Marekani na kuwaalika watu kusherehekea pamoja naye, sherehe hizo zilifanyika usiku na mchana ndani ya boti kwa pesa za umma, kwa uamuzi wake mwenyewe, Florence alikuwa akiwaalika waandishi wa habari na kuwafanyia tafrija ya siri Ikulu, akila na kunywa nao, alifanya hivyo kuhakikisha anawaweka karibu, wawe wanampamba kuwa yeye ni First Lady bora kuwahi kutokea, vilevile kuuzungumzia vizuri utawala wa mume wake, Florence alikuwa mke wa Rais wa Marekani ambaye alikuwa na utaratibu wa kufanya mikutano na waandishi wa habari pamoja na kulihutubia taifa mara kwa mara kuliko mume wake yani yeye ndie aligeuka kuwa rais.

Kubwa zaidi ni kwamba pale alipo taka kujua kila kitu kwenye jamii na ndani ya Serikali ya mume wake, Florence wakati mwingine alijifanya shushushu, vilevile alitoa maelekezo kwa taasisi za ujasusi ili zimtafutie alichotaka, vitimbi vya Florence haviishii hapo, kingine ni kuwa aliamini sana ushirikina, wakati mwingine aliwaalika Ikulu wapiga ramli na wanajimu (fortunetellers and astrologers) na kuwataka wambashirie mambo yajayo, vilevile wamweleze mambo ya giza ambayo yalikuwa yakimzunguka nchini, yeah unashangaa kusikia uchawi mamtoni ndio hivyo utake ndio hivyo usitake ndio hivyo.

Kitabu kilichaondikwa na mwandishi Carl Sferrazza Anthony, kinachotwa "Florence Harding (The First Lady, the Jazz Age, and the Death of America's Most Scandalous President)" ,ndani yake yameelezwa mengi kuhusu Florence unaweza kuona namna alivyo kuwa iron women and rubbish women kwa wakati mmoja, unajua Florence alikuwa na kiburi kwakuwa yeye ndiye aliyecheza nafasi muhimu kumfanya mume wake kuwa Rais, kwani alifanya kuwa hero kutoka kwenye hatua ya mwanzoni alionekana mgombea dhaifu, jambo hili ndilo ambalo linamfanya Florence kuwa na sauti kuliko mume wake baada ya kushinda urais, ni Florence aliyemnyang’anya Harding simu, alipokuwa anampigia kampeni meneja wake, Harry Daugherty kumweleza dhamira yake ya kujitoa, baada ya hapo Florence alikata simu, Harding ilibidi asalimu amri kwa mke wake, akamwambia: “Sawa, basi nisaidie kuwambia Harry Daugherty kuwa tutapambana mpaka barafu la Jehanamu liyeyuke.”

Unajua mwaka 1920 ulikuwa wa bahati kwa Harding, maana aliokota dodo chini ya papai dume, inawezekana nyota ya mke wake nayo ilichangia, hivi unajua kuwa mke nae ni daraja la mafanikio yako? Kama hujui ngoja nikujuze sasa, inawezekana mke wako akawa sababu ya wewe kuwa raisi, ebu Soma kisa cha Michael Obama, alikuwa na ndoto za kuwa mke wa raisi... Unadhani bila Michael Obama Barack Obama angekuwa rais? Najua ujanielewa hapo, lakini ukweli ni kwamba hata Abraham Lincoln asingekuwa rais bila mkewe Tody Lincoln.

Unajua kuwa ule uchaguzi wa 1920 aliyekuwa anapewa nafasi kubwa ya kushinda tiketi ya Republican, alikuwa Rais wa zamani wa nchi hiyo kati ya mwaka 19011 mpaka 19019, Theodore Roosevelt, aliyekuwa anataka kuongoza taifa hilo kwa kipindi cha tatu? hata hivyo, Roosevelt alifariki dunia ghafla Januari 6, 1919, hivyo kuacha mlango wazi, wakajitokeza wagombea kadhaa akiwemo Jenerali mstaafu wa Jeshi la Marekani, Leonard Wood, aliyekuwa Gavana wa Illinois, Frank Lowden, Seneta wa California, Hiram Johnson, Rais wa baadaye wa nchi hiyo, Herbert Hoover, Gavana wa Massachusetts, Calvin Coolidge, Jenerali John Pershing na Warren Harding mwenyewe, hata hivyo Desemba 17, 1919, Harding alipotoa tangazo la kuwania tiketi ya kuwa mgombea urais kupitia Republican, watu walimwona kama anakwenda kusindikiza, na kweli matokeo ya jumla yalipotoka, kuelekea mkutano mkuu wa chama, Harding alikuwa wa sita kwa kura yani kushika mkia.

Hivyo Florence alitumia gazeti lao la familia, linaloitwa The Marion Star kumpamba mume wake na kuwashambulia wapinzani wake, huyu huyu Florence pia ndiye aliyemsaidia Harding alipogombea useneta wa Ohio mwaka 1914 na kumwewezesha kushinda, alimsaidia katika usimamizi wa fedha na mvuto wa kijamii, kweli mke akiamua huwezi kushindwa ebu jaribu kukumbuka kampeni za Kikwete mwaka 2010 namna mama Salma alivyo pambana kumfanya kikwete kushinda huu ndio usawa katika utafutaji, sio kutafuta atafute mwanamme alafu kula ale mwanamke, utasikia tuma nauli, Loh! Sijui ujinga huu wanawake wamefunzwa na nani.

Florence alikuwa tofauti na mademu wa siku hizi, alitumia umaharufu wake na pesa zake kwenye mambo ya maana sio kama hao wakina Amber lutt sijui Wema Sepetu wamekalia umaarufu wa kishamba, kwa Florence alikuwa maarufu na jina lake lilitosha kumwombea kura mume wake, hivyo basi, kama ambavyo alimsaidia Harding kushinda useneta wa Ohio, ndivyo jina lake lilivyombeba Harding katika mbio za urais, baada ya Harding kutoka wa sita, walielekea kwenye mkutano mkuu wa taifa (1920 Republican National Convention), ghafla hali ya hewa ilichafuka, mgawanyiko mkubwa ulitokea, Kashfa ya watu kutumia fedha kununua wajumbe ilirindima, baada ya hapo ukafuata uchunguzi ambao ripoti yake ilipokamilika, ilibainisha kuwa Wood alitumia Dola1.8 milioni ambazo kwa sarafu ya sasa ni Sh4 bilioni, Lowden alitumia Dola600,000 (Sh1.3 bilioni), Johnson Dola194,000 (Sh400 milioni), Harding alionekana kutumia kiasi kidogo zaidi, Dola113,000 (Sh227 milioni) siunajua sheria za Marekani huzuia matumizi makubwa ya pesa kwenye kampeni zao Ehhh! Wao sio sisi waafrika ndio maana waswahili husema penye miti hapana wajenzi

Florence aliitumia ripoti hiyo kuwaonesha wagombea wengine kuwa wananunua urais, kampeni kubwa ikawa inafanywa kuwa Harding awe mgombea kwa sababu ndiye aliyetumia fedha kidogo kuliko wengine, Juni 11, 1920, kura za mkutano mkuu zilipigwa lakini hakuna hata mmoja aliyefikisha kura 498 zilizohitajika ili atangazwe mgombea. Wood alipata 314, Lowden 289 na Harding alipata 65, usiku wa Juni 11 mpaka 12, 1920, historia iliandikwa, pale wazee wa chama (party elders) walipojitokeza kuwalazimisha wajumbe wa mkutano mkuu wa Republican kumchagua Harding ili kukitetea chama kisigawanyike, Kutokana na shinikizo la wazee, wajumbe wa mkutano kwa kura nyingi walimchagua Warren Harding kuwa mgombea urais wa Republican, tukio ambalo liliweka historia kwa sababu hakuwa amefikiriwa kabla.

Shukurani za ushindi huo zinakwenda kwa Florence ambaye mbali na gazeti lake kutumika kuchafua wagombea wengine pamoja na kumpamba Harding, vilevile alipenya kwa watu muhimu kwenye chama na kuwashawishi wazee kumkubali Harding, hapa ndio Florence alipata wigo wa kuikamata ikulu na kumkamata mmewe.

Florence alikuwa mkubwa kwa Harding kwa miaka mitano, kwani Florence alipofunga ndoa na Harding, ilikuwa ndoa yake ya pili, Mwaka 1880, Florence akiwa na umri wa miaka 20, aliolewa na mume wake wa kwanza, Henry DeWolfe na kuzaa naye mtoto mmoja wa kiume, Mwaka 1886 waliachana, kisha mwaka 1891 alifunga ndoa na Harding, wakati huo, Harding alikuwa mjasiriamali, akimiliki gazeti la The Marion Star, Baada ya ndoa yao, Florence alishika nafasi ya uongozi wa gazeti hilo na ndipo gazeti hilo lilopo anza kupata mafanikio kwa kuchapa nakala nyingi, baada ya kushika uongozi wa gazeti hilo, ndipo Florence alipodhihirisha uwezo wake wa kuongoza gazeti, umaarufu wake binafsi ulipaa zaidi, vilevile umaarufu wa gazeti uliongezeka, umaarufu wa Florence ulikuwa mtaji mkubwa kwa Harding baada ya kuteuliwa na Republican, kwani mwanamke huyo alifanya kampeni ya nguvu, kwani yalikuwepo maneno kwamba Harding alishinda urais si kwa sababu nyingine, bali kuwa mume wa Florence.

Lakini huyu Florence baada ya mume wake kushinda akamtaabisha, Florence akawa akamatiki tena akawa jini liloondolewa kwenye chupa, nani wakulirudisha tena? Kila mtu akamgwaya! unajua lakini kuwa Florence alikuwa moto wa kuotea mbali? hata mmewe alifunga kinywa, kwa bahati mbaya mume wake akutawala sana, utawala wake uliongoza kwa miaka miwili na nusu tu, kwani Agosti 2, 1923, Harding alifariki dunia baada ya kuiongoza nchi hiyo kwa miaka miwili na nusu, kifo cha Harding kilijaa utata mkubwa, Ikavumishwa kuwa Florence alimpa sumu Harding kwa sababu za wivu wa mapenzi, uvumi huo ukapata nguvu kufatia msimamo wa Florence kukataa mwili wa Harding usifanyiwe uchunguzi kubaini kilichomuua, ulisababisha maneno mengi zaidi kuvumishwa kuwa alimpa sumu baada ya kubaini ana uhusiano na mwanamke mwingine.

Lakini wengine walipiga hili la Florence kumpa sumu mme wake, upande huu ulidai kuwa Warren Harding alikuwa mgonjwa wa muda mrefu kwani wakati mchakato wa Republican ulipoanza, Harding alionekana kuwa mgombea dhaifu kiafya, hata aliyekuwa mtabiri maarufu wa Marekani kipindi hicho, Madame Marcia Champrey, alimtabiria Harding kushinda urais lakini akasema pia kuwa angekufa kabla ya kumaliza muhula wake mmoja wa miaka minne, hata pale Florence alipokataa mwili wa mume wake usifanyiwe uchunguzi, alikuwa akisisitiza watu kuheshimu utabiri wa Madame Marcia kuwa Harding angeshinda urais kisha angekufa akiwa madarakani, kweli Florence alikuwa na roho ngumu kweli, Hata hivyo, baada ya kifo cha mumewe Florence hakufikishwa mahakamani, taarifa zilidai alikufa kwa shambulio la moyo, zipo nyingine zilieleza ni sumu, japo hili la sumu lilipewa uzito sana kwa watu.

Baada ya kifo cha Harding, Florence aliishi mwaka mmoja na miezi mitatu tu, kwani Novemba 21, 1924, naye alifariki dunia, hapa ndio ujue kwamba ngoma ikivuma sana lazima ipasuke, huyu Florence aliyemuingiza mume wake Ikulu, kisha akaitumia White House kama mali yake, hakutosheke kumkamata mumewe katika Limbwata, wivu ukamjaa akaona mumewe kavuka mipaka akamuua, mapenzi ni hatari lakini wanawake ni hatari zaidi, alipewa ikulu yote kwa kipindi cha miaka miwili na nusu lakini bado akuridhika, akaona limbwata halitoshi akaona amfyekele mbali mpenzi wake aliye sota usiku na mchana kumpambani afanikiwe, kweli mapenzi ya kupendana sana yana limbwata kali sana.

[emoji117][emoji420]Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
[emoji2400]Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
[emoji2398] Copyrights of this article reserved
[emoji2400]written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
[emoji769]Comred Mbwana Allyamtu
Kwa Tanzania
+255679555526.
+255765026057.

Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234

Kwa DRC
+243 977 860 824
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com

[emoji2398] Copyright 2019, All Rights Reserved.
 
Back
Top Bottom