Limekaaje hili la diploma to digree...


Mkuu sifikiri kama chuo cha serikali kitakuwa kinapromote njia za mkato. Utaratibu ulivo duniani kote hasa ni level ya chini katika chuo ni certificate (1 year) diploma (2 yrs) bachelor(3/4yrs), na sijawahi kusikia katika nchi yoyote yenye utaratibu usemao kuwa baada ya diploma, mtu akae nje mwaka mzima!!! Huku ni kurudishana nyuma! Ingekua vile vyuo vya kihindi vya kila course miezi sita kweli, lakini chuo cha serikali, kilichoweka ngazi hizo kisha eti ukae nje mwaka mzima!! Mwaka mzima ufanye nini? Sasa kwa mfumo huo wakukaa nje mwaka mzima ndo utazalisha MIFISADI hasa ilobobea!! Tz hakuna elimu, ndo maana watu hukimbilia India na malaysia!
 
Ukweli utabaki palepale kama TCU/NACTE watakubali hicho chuo chenu kidahili wanafunza wa kuunganisha hapo sawa,lakini maelezo ya kuwa wanafunzi wa diploma inabidi wasubiri kwa miezi kadhaa unategemeana na academic year ya vyuo vya tz ilivyo,wanafunzi wa certificate na diploma wanaanza chuo mwezikuanzia mwezi wa nane hadi wa kumi,kumaliza mwaka ni mwezi wa sita au wa saba,masahihisho ya mitihani ni zaidi ya miezi miwili ie hadi mwezi wa nane au tisa,muda ambao mwaka mpya wa masomo ndio unakuwa umeanza,so kinachobakia hapo ni makubaliano kati ya chuo na taasisi zinazosimamia udahili ie TCU/NACTE kama watakubali,tofauti na hapo inabidi usubiri!
 

dah! Kama mpango ndio huu siku hizi basi nchi itakwenda kuzalisha maharamia sugu.mwako mmoja ni mrefu sana jamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…