Linah akanusha taarifa za kujifungua

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Msanii Linah Sanga 'Ndege Mnana' amekanusha taarifa zinazoenea mtandaoni kuhusu suala la kujifungua na kuwataka watu wazipuuzie huku akiwasihi mashabiki zake waendeee kusubiri taarifa iliyo sahihi kutoka kwake na kwenye mitandao yake ya kijamii.

Linah amekanusha taarifa hizo kupitia EATV na kusema kwamba anashangazwa na taarifa zinazosambaa mitandaoni huku akiwa hajui mtu anayesambaza taarifa hizo ana malengo gani.

"Hongera ya nini mbona mimi bado mjamzito? Sijajifungua bado na hata mwenyewe nashangazwa na huyo mtu aliyeanza kusambaza taarifa hizo ana malengo gani? Nawaomba mashabiki zangu waniombee kwa sasa hivi nikiwa nakaribia kwenda kujifungua hivi karibuni ingawa siwezi kusema ni lini kwani siyo vizuri, watu wanatakiwa waone. Mungu akinisaidia taarifa watazipata kupitia kwangu mwenyewe au kwenye mitandao yangu ya kijamii," Linah alifunguka .

Katika hatua nyingine Linna ameongeza kwamba sababu ya za kutoonekana sana kipindi cha hivi karibuni hakujasababishwa na kisirani, hivyo kutoonekana kwake zipo sababu ya msingi.

"Ukweli nina sababu zangu za msingi zinazonifanya nisionekane, Ninachomshukuru Mungu kuwa na mimba hakujanifanya niwe kisirani ila baada ya ya sababu zangu kuisha nitaonekana kama kawaida. Niombeeni nijifungue salama", aliongeza

EATV inamuombea mwanamuziki Linah maandalizi mema ya kumpokea mtoto wake wa kwanza.
 
Basi sawa tunasubiri

Sent from my Apple iPhone 5s using JamiiForums Auto-reply Mobile app
 
ilaaaa naye amekaaa mudaa mrefu jaman khaaaa, mpkaa tushamsahau kama mjamzito yaan wamama wote aliobebaa nao mimbaa washajifunguaaa kabak yeye tu,mmmh au ukute yule mwenzie kamfanyiziaa manake sidhan kama alifurahiaa kunyanganywa tonge mdomoni,kumchukuaa mchumbaa wa MTU ni kitu kibayaa saanaa!
 
Mpaka leo hajajifunga duuuh kama mimba ya tembo, huyo mtoto atakua kishaota meno huko tumboni
 
Mpaka leo hajajifunga duuuh kama mimba ya tembo, huyo mtoto atakua kishaota meno huko tumboni
[emoji23] [emoji23] [emoji23] wabongo mna majungu dahh..

Kweli JF sihami

Sent from my Iphone 7 using JamiiForums mobile app
 
Inawezekana tumbo lake lilitanuka mapema
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] wabongo mna majungu dahh..

Kweli JF sihami

Sent from my Iphone 7 using JamiiForums mobile app
Serious nimeshangaa, nlijua mtoto atakua anatambaa chinekeeee
 
U Beyonce unawaponza watu .....this is Africa ....

All the best linah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…