Yussufhaji
Member
- Sep 9, 2018
- 35
- 28
“MATAIFA MAKUBWA HUWA HAYANA SIMILE”
24/02/2022
Ni nani asiyejuwa kinachoendelea nyuma ya pazia la mapinduzi ya kila siku yasiokwisha Afrika ya Magharibi?
Wangapi wamesahau kikosi cha jeshi la Ufaransa kilipovamia Ivory coast na kumtoa madarakani Laurent Gbabo pale alipo goma kumkabidhi madaraka mpinzani wake kwa kisingizio cha kulinda demokrasia na utawala wa sheria?
Wangapi tunakumbuka Sadam Hussein alivyoondolewa madarakani na vikosi vya NATO na washirika wake bila ya simile kwa hoja ya kuwepo kwa silaha za nyuklia nchini Iraq jambo ambalo uchunguzi wa Umoja wa Mataifa ulionyesha kukanusha kuwepo kwa silaha hizo nchini Iraq?
Mwaka 2011 dunia ilishuhudia Ufaransa, Marekani na washirika wao wa NATO kutokuwa na simile walipoishambulia Libya hadi kumtoa Canal Muammar Gaddafi madarakani sababu ikiwa ni kuwaunga mkono raia wa nchi hiyo na kuwalinda,
Historia inaonyesha Taiwan kuwa ni sehemu ya China, lakini baada ya kibaraka wa Marekani Ching Kai-shek kuondolewa China bara na Mao Zedong na kukimbilia katika visiwa vya Taiwan na serikali yake huku akiitangaza Taiwan ni nchi iliyojitenga na China bara, Marekani na washirika wake hawakuwa na simile kuitambua serikali hiyo kwa kulinda maslahi yao,
Wote tunashuhudia katika mgogoro wa Yemen jinsi gani dola zenye nguvu na ushawishi Mashariki ya Kati zinavyohaingaika kuweka serikali itakayowanufaisha wao nchini humo,
Tukio hili la Urusi kuyatambua majimbo yanayotaka kujitenga Donetsk na Luhansk nchini Ukraine na kutuma vikosi vyake nchini humo huku iki iambia dunia inakwenda kulinda amani nchini humo yanikumbusha mzozo wa kinyuklia wa mwaka 1962,
Nini hasa kilichotokea 1962? Mzozo huu wa kinyuklia maarufu “Cuba missile crisis” ulichochewa na hatua ya Marekani kuweka silaha za nyuklia nchini Uturuki na Italy huku ikiwa tishio kwa maslahi ya kiusalama ya lililokuwa shirikisho la kikomunisti la wa soviet (USSR) ambapo katika kujibu mapigo, USSR iliamua kuweka silaha za nyuklia chini ya pua ya Marekani, Cuba. Ambapo Marekani ilihadhabishwa zaidi na hatua hiyo ya USSR kuweka silaha za nyuklia Cuba na kuamua kutishia kuiripua mizinga hiyo ya nyuklia iliyopo Cuba kama haito ondoshwa pasi ya kuwa na simile kwani ni tishio kwa maslahi ya usalama wa Marekani,
Na ndio hivyo hivyo Urusi inavyoona kwa Ukraine iwapo itakuwa mwanachama wa umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi NATO basi maslahi yake yakiusalama yatakuwa yameguswa moja kwa moja,
Hatua inazo zichukuwa Urusi hivi sasa dhidi ya Ukraine ni kulinda maslahi yake ya kiusalama yaliyoguswa na NATO na Ukraine, hivyo Urusi inaonekana kutokuwa na simile na sheria za kimataifa wala uhuru wa Ukraine kwasababu tu ya kuguswa maslahi yake ya kiusalama,
Inachokifanya Urusi kwa Ukraine ndivyo wafanyavyo mabwana wa dunia/madola makubwa (superpowers) pale maslahi yao yanapoguswa.
Hakuna jipya, wala la kushangaza, ni muendelezo wa desturi na tamaduni za madola hayo.
NB: Maoni yangu binafsi kwa kile kinachoitwa “Mzozo wa Ukraine”
@Mtoto_wa_Mkulima
Email: hajjyussuf2@gmail.com
Simu: +255777158131