"Linda utajiri wako, ogopa umasikini " Mzee Abdul

"Linda utajiri wako, ogopa umasikini " Mzee Abdul

Wakuu hapa simlaumu Diamond wala Mama yake, Kuna siri kubwa ndani ya hii familia.
Naamini kabisa DIamond na pesa zake asingeshindwa kumsaidia huyu mzee huku akiwsaidia watu baki asiowajua.

FUNZO KWA WANAUME WENZANGU:
Mnapokuwa na kipato acheni kutelekeza na kunyanyasa familia zenu.
Hapa wote mnaonekana kumuonea huruma, mnajua kiindi ana maisha mazuri alikuaje?
 
Qmmke umaskini ni kitu kibaya sana kwa Mwanaume ndo maana tunavuka mipaka ya kutafuta pesa, utadhalilishwa hadi na Mende & Panya maana huna uwezo wa kuwaua
 
Kauli hii wanaume tuiweke katika sehemu salama zaidi katika vichwa vyetu. Maneno ya mwisho ya Mzee Abdul kumuasa aliyekua mwanae kuhusu maisha.
Binafsi mimi simfuatiliaji sana wa haya mambo ya macelebrities lakini siku mbili nimeusikia mjadala huyu.
Kwa haraka haraka shida kubwa iko kwa mama yake Diamond na nahisi kuna "kaulimbukeni fulani".Kwa mila za kiafrika aliyekulelea mtoto ndiye baba yake hata kama sio biological father,Ashakum si matusi "kutia/kutiwa mimba ni starehe" lakini kuelea mtoto ni kazi kubwa.Hata kama wangehilitilafiana vipi kauli hii haikustahili.
Jambo la pili kwa Mama Diamond ni kujitahidi kufungua macho kwani katika watu ambao wanaanguka na kudhalilika vibaya ni wanamuziki na wanamichezo.Hatutashangaa tukimuona Diamond ana pack juice kwenye kiwanda cha Mhindi.Akae atulie!!
 
Back
Top Bottom