Baada ya member wa JamiiForums.com kuleza kuwa anakerwa na usumbufu wa uwepo wa mbu wengi katika Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi, hatua zimeanza kuchukuliwa kwa kufanya usafi.
Afisa Afya Wilaya ya Nachingwea, Joseph Masia amekiri Hospitali hiyo kuwa na Mbu wengi na hivyo wanachofanya kwa sasa ni usafi wa mazingira na kuondo mazingira yote yanayochangia wadudu hao kuzaliana kwa wingi