LGE2024 Lindi: CCM na CUF wafungana Matokeo ya Uchaguzi Liwale, Uchaguzi kurudiwa

LGE2024 Lindi: CCM na CUF wafungana Matokeo ya Uchaguzi Liwale, Uchaguzi kurudiwa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

1732814682417.png

Msimamizi wa uchaguzi wa halmashauri ya Liwale, Tina Sekambo, ametangaza rasmi matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa leo, Novemba 28, 2024, ofisini kwake, mbele ya waandishi wa habari.

Katika taarifa yake, Sekambo ameleza kuwa halmashauri ya Liwale inajumla ya vijiji 76 na vitongoji 351, ambapo kwa mujibu wa matokeo, chama cha CCM kimeibuka kinara kwa kushinda katika vijiji vyote 76 na vitongoji 349, huku chama cha CUF kikiibuka na ushindi katika kitongoji kimoja pekee.

Hata hivyo, alibainisha kuwa katika kitongoji cha Jamhuri kilichopo katika Kijiji cha Mbaya, Kata ya Mbaya, hali ya uchaguzi ilivyojiri ilionyesha matokeo ya kifungamano kati ya wagombea wa CCM na CUF.

Kutokana na hilo, Msimamizi wa Uchaguzi alitangaza kuwa uchaguzi katika kitongoji hicho utarudiwa Novemba 29, 2024.

PIA SOMA
- LGE2024 - Lindi: Msimamizi wa Uchaguzi kwenye Manispaa asisitiza wagombea kufanya kampeni za kistaarabu
 
Back
Top Bottom