Pre GE2025 Lindi: CHADEMA yazungumza kukamatwa kwa Steven Membe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

1732510795990.png

Taarifa za kukamatwa na kisha kushikiliwa kwa Steven Membe ambaye pia ni mtia nia wa kuwania Ubunge wa jimbo la Mtama, Lindi kupitia CHADEMA katika uchaguzi mkuu ujao (2025) zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii hatua ambayo iliibua maswali na sintofahamu huku kukiwa na hisia mseto zinazodai kuwa huenda kukamatwa kwake kunatokana na mikutano ya hadhara ya chama hicho aliyoifanya hivi karibuni akiwanadi wagombea wa chama chake wanaopeperusha bendera kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024

Jambo TV imezungumza kwa njia ya simu na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kusini Governor Kaduma ambaye amesema kuwa Steven Membe amekamatwa tangu Ijumaa ya Novemba 22.2024 asubuhi akiwa nyumbani kwake kijiji cha Chiponda, kata ya Chiponda, tarafa ya Rondo, jimbo la Mtama, wilaya na mkoa wa Lindi, akidai kuwa hiyo ni mara ya pili kukamatwa kwa siku za hivi karibuni

Kupata nyuzi za kimkoa Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Amesema baada ya kupata taarifa hizo, viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakifanya jitihada za kuhakikisha wanamtoa angalau kwa dhamana lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida maafisa wa Polisi waliomkamata wanadai kuwa wao hawana mamlaka ya kumpatia dhamana kutokana na kile kilichoelezwa kuwa jambo hilo linashughulikiwa moja kwa moja na Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi

Kutokana na ukweli kwamba kutoka Ijumaa hadi sasa ni zaidi ya saa 24 za kisheria walizopewa Jeshi la Polisi kukaa na mtuhumiwa bila kumfikisha Mahakamani au kumpatia dhamana, viongozi hao wa CHADEMA wamesema wamesema wameambiwa kuwa Jumatatu hii ya Novemba 25.2024 atafikishwa Mahakamani

Aidha, Katibu huyo wa CHADEMA Kanda ya Kusini Governor Kaduma amesema licha ya kwamba hawajaelezwa ni Mahakama ipi atapelekwa na muda gani lakini wao wameshawaandaa Mawakili watakaohakikisha wanafuatilia kwa karibu jambo hilo, na kwamba endapo Jeshi la Polisi halitomfikisha Mahakamani wao hawatakuwa tayari kuendelea kushuhudia sheria na Haki za Binadamu 'zikikanyagwa'...

Pia soma
- LGE2024 - Polisi wamkamata na kumuweka Lock up Steven Membe, Mwanachama wa CHADEMA, nyumbani kwao Rondo
 
Anaenda kumpinga Princess wa Korosho......hilo ndio kosa kubwaaa
 
Pale law enforcment inapovunja rule of laws kwa makusudi. Unajiuliza huo utii wa sheria bila shuruti ni kwa wananchi tu? Mbona wao hawazitii?
 
Ndugu yake Membe aliyemwachia jimbo Nape??
 
Ukishakuwa upinzani, jiandae kwa figisu...
 
Isije ikawa polisi wamemuua tayari ndiyo maana hawataki kutoa dhamana kwa vile hayupo tena duniani.
 
Nape aanze kufungasha kwenda kwao kand ya ziwa maana wenyeji wa Mtama wanamtaka mtoto wao awaongoze na bao la mkono hali nafasi na kupita bila kupingwa hakupo tene.
 
Wakuu,

Taarifa za kukamatwa na kisha kushikiliwa kwa Steven Membe ambaye pia ni mtia nia wa kuwania Ubunge wa jimbo la Mtama, Lindi kupitia CHADEMA katika uchaguzi mkuu ujao (2025) zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii hatua ambayo iliibua maswali na sintofahamu huku kukiwa na hisia mseto zinazodai kuwa huenda kukamatwa kwake kunatokana na mikutano ya hadhara ya chama hicho aliyoifanya hivi karibuni akiwanadi wagombea wa chama chake wanaopeperusha bendera kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024

Jambo TV imezungumza kwa njia ya simu na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kusini Governor Kaduma ambaye amesema kuwa Steven Membe amekamatwa tangu Ijumaa ya Novemba 22.2024 asubuhi akiwa nyumbani kwake kijiji cha Chiponda, kata ya Chiponda, tarafa ya Rondo, jimbo la Mtama, wilaya na mkoa wa Lindi, akidai kuwa hiyo ni mara ya pili kukamatwa kwa siku za hivi karibuni

Amesema baada ya kupata taarifa hizo, viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakifanya jitihada za kuhakikisha wanamtoa angalau kwa dhamana lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida maafisa wa Polisi waliomkamata wanadai kuwa wao hawana mamlaka ya kumpatia dhamana kutokana na kile kilichoelezwa kuwa jambo hilo linashughulikiwa moja kwa moja na Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi

Kutokana na ukweli kwamba kutoka Ijumaa hadi sasa ni zaidi ya saa 24 za kisheria walizopewa Jeshi la Polisi kukaa na mtuhumiwa bila kumfikisha Mahakamani au kumpatia dhamana, viongozi hao wa CHADEMA wamesema wamesema wameambiwa kuwa Jumatatu hii ya Novemba 25.2024 atafikishwa Mahakamani

Aidha, Katibu huyo wa CHADEMA Kanda ya Kusini Governor Kaduma amesema licha ya kwamba hawajaelezwa ni Mahakama ipi atapelekwa na muda gani lakini wao wameshawaandaa Mawakili watakaohakikisha wanafuatilia kwa karibu jambo hilo, na kwamba endapo Jeshi la Polisi halitomfikisha Mahakamani wao hawatakuwa tayari kuendelea kushuhudia sheria na Haki za Binadamu 'zikikanyagwa'...

Pia soma
- LGE2024 - Polisi wamkamata na kumuweka Lock up Steven Membe, Mwanachama wa CHADEMA, nyumbani kwao Rondo
Goli la mkono ana wasiwasi ???!!
 
Back
Top Bottom