Uchaguzi 2020 Lindi: Majengo ya Serikali yachomwa, magari yaharibiwa kisa Uchaguzi

Uchaguzi 2020 Lindi: Majengo ya Serikali yachomwa, magari yaharibiwa kisa Uchaguzi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mkuu wa Mkoa huo, Godfrey Zambi, ameyaeleza hayo mjini Lindi, alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na uharibifu uliofanywa wakati wa uchaguzi mkuu Oktoba 28, mwaka huu.

Watu hao wanadaiwa kufanya fujo kwa sababu ya kutoridhishwa na mwenendo wa uchaguzi ulivyokwenda, kutokana na kile kinachodaiwa kuhujumiwa, ikiwamo kuzuiliwa mawakala kuingia vituoni, ongezeko la vituo hewa vilivyo nje ya mfumo na vitambulisho vya kupigia kura.

Madai mengine ni kubadilishiwa matokeo ya ushindi ya mgombea aliyeshinda kupewa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Zambi alisema katika fujo hizo, magari zaidi ya saba kati ya hayo mawili ya polisi, majengo ya serikali pamoja na binafsi tisa na pikipiki moja, yaliharibiwa kwa kuchomwa moto.

Zambi alizitaja wilaya zilizoathirika kutokana na uharibifu huo ni Liwale, Nachingwea, Kilwa na Lindi katika Halmashauri ya Mtama.

Amesema Liwale magari zaidi ya saba, likiwamo la polisi na binafsi yaliyokodiwa kusaidia uchaguzi huo, yaliharibiwa, na kwamba nyumba mbili na magari matatu ya Mbunge mteule, Mohamed Kuchauka.

Imo pia zahanati ya Diwani mteule Kata ya Liwale Mjini, Omari Mkoyage na nyumba moja ya askari polisi.

Zambi alisema wilayani Nachingwea, magari matatu na nyumba, mali za Diwani mteule Ahamadi Makoroganya, gari moja la polisi na nyumba zimechomwa moto, huku jengo la Mahakama Wilaya limenusurika licha ya kuwamo kwenye orodha ya kutaka kuichoma.

Kwa mujibu wa Zambi, Halmashauri ya Mtama, watu hao walichoma moto majengo mawili, ikiwamo ofisi ya muda anayoitumia Mkurugenzi Mtendaji, Samuel Waryoba, Ofisi ya Serikali ya Kata ya Mtene na jengo la saluni la mtendaji wa kata hiyo.

Alisema Jeshi la Polisi linawashikilia watu kadhaa kwa ajili ya mahojiano, kwa lengo la kuwabaini waliohusika.

CHANZO: Nipashe | Mwandishi - Said Hamdani
 
Wizi na hujuma za demokrasia nchini, haziwezi kudhibitiwa kwa maandamamano ya Lissu, Mbowe na Zitto. Lindi wameonesha mifano japo kwa asilimia 20% walitakiwa wafike 80% ya kudai democracy.

Kumbuka, CCM wanafaidika na wizi huo. Hawako tayari kuziachia faida hizo. Na wananchi nao hawako tayari kuandamana eti kisa kudai democracy. Yapaswa wale walioumizwa kuwatafuta wote waliowaumiza na kulipa kisasi, yaani malipo yawe hapahapa.

Kuna aliyewaapisha walinzi kulinda wasimamizi.
Kuna aliyenyima barua za mawakala
Kuna waliosimamia na kutekeleza walichoagizwa na yule wa kwanza.

Hawa wote yafaa wapate maumivu ya kuharibu uchaguzi. La sivyo mmewapa kibali cha kula mema ya Tanzania kwa miaka mitano tena. Na watafanya ni kawaida.

Lindi wameonesha njia
 
Kama ni kweli basi inaelekea picha na majina ya wagombea wa CCM ndio yaliyokua akilini na mioyoni mwao
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hahaha uongo huu, juzi walisema Mtwara hali tete, leo wanatuletea habari za Lindi.

Mi nitasubiria kuona moto kwa macho yangu hapa Dar es Salaam, kama sitauona basi najua zote hizi ni story za kutengeneza.
 
Back
Top Bottom