The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Rukia Said akikadiliwa kuwa na umri wa miaka 25-30 amekutwa na umauti ndani ya basi la abiria akisafirishwa kutoka Kilwa Pande kuelekea Hospitali ya Rufaa mkoani Lindi - Sokoine kwa lengo la kupatiwa matibabu.
Katika Hali isiyo ya kawaida mwili wa marehemu umekataliwa kuingia ndani ya Hospitali hiyo na kutelekezwa barabarani kabla ya mvua kunyeshea mwili huo huku ndugu wakihaha kuomba msaada kutoka kwa wasamalia wema ili kurejea makwao kwa shughuli za mazishi.
Ndugu wa marehemu Zakia Yusuph na mashuhuda wa tukio hilo lililojiri leo Machi 11, 2025 akiwemo Tausi Jafari na Abdallah Mtaji ambaye ni miongoni mwa wasafiri walioambatana na marehemu kutoka Kilwa, wameeleza kusikitishwa kwa kitendo kilichooneshwa na wahudumu wa Hospitali hiyo huku sababu za kukataliwa kwa mwili ikitajwa kuwa ni kukosekana kwa kitanda cha kubeba mwili na kuingizwa mochwari jambo ambalo liliondosha matumaini ya kupatiwa huduma.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine Dkt. Shadrack Msasi amekiri kutokea kwa jambo hilo lililosababishwa na ndugu wa marehemu kutopewa taarifa sahihi na kueleza kuwa hata hivyo mwili ulitakiwa kupokewa geti kubwa walipofika watu hao kwa mara ya kwanza na baadae kufanyiwa vipimo kabla ya kupelekwa mochwari.
Aidha, amekana taarifa ya kukosekana kwa vitanda katika Hospitali hiyo kama taarifa zilizovyotolewa na wahudumu na kuongeza kuwa, vifaa vyote vinapatikana na huduma zote za msingi zinatolewa kwa uhakika.
Mpaka mwili wa marehemu unaondolewa eneo la Tukio bila ya huduma yoyote, wasamalia wema wakiongozwa na jopo la madereva wa bodaboda Manispaa ya Lindi wamekusanya kiasi cha shilingi 101,100/= zilizokabidhiwa kwa ndugu pamoja na jeneza ili kuhifadhi mwili wakati na baada ya kurejea makwao.