LGE2024 Lindi: Matukio yaliyojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024

LGE2024 Lindi: Matukio yaliyojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

WanaJF,​

Mada hii itakuwa na 'Updates' za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Lindi. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kushiriki na wengine.

1727773525137.jpeg

Ramani ya Mkoa wa Lindi

Historia ya Mkoa wa Lindi
Mwaka 1961 wakati Tanganyika inapata Uhuru wake kutoka kwa Waingereza Mkoa wa Lindi haukuwapo kabisa katika ramani. Kilichokuwapo wakati huo ni Jimbo la Kusini ambalo lilijumuisha Mikoa ya sasa ya Lindi Mtwara na Ruvuma. Makao Makuu ya Jimbo hilo la Kusini yalikuwa katika Mji wa Lindi. Hadhi ya Mji wa Lindi kuwa Makao Makuu iliishia mara baada ya Uhuru ambapo Jimbo la Kusini likawa linajulikana kama Mkoa wa Mtwara. Makao Makuu yakawa ni Mji wa Mtwara. Yamkini Mkoa wa Mtwara ulikuwa mkubwa sana kwa eneo hata Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Mtwara Bwana John Nzunda alikuwa anasema:

“Natawala kipande cha nchi toka Pwani ya Bahari ya Hindi hadi Ziwa Nyasa na kutoka Mto Ruvuma hadi karibu na mto Rufiji.” Serikali wa awamu ya kwanza Iliyoongozwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliugawa Mkoa wa Mtwara miaka ya mwanzo ya Uhuru ambapo kukawa na Mikoa ya Mtwara na Ruvuma. Mgawanyiko huu uliifanya Lindi kuwa ndani ya Mtwara.

Julai 1, 1971 ndipo Mkoa wa Lindi ulianzishwa rasmi baada ya tena kuugawa Mkoa wa Mtwara. Makao Makuu ya Mkoa yakawa Mji wa Lindi. Wakati Tanzania inaadhimisha Miaka 10 ya Uhuru wa Bara kwa kuwaita Waingereza kuja kuiona hatua iliyopiga Mkoa ulikuwa na umri wa miezi 6 tu.

MUHTASARI WA MAENEO YA UTAWALA LINDI
1727773634135.png

CHANZO CHA TAKWIMU: TAMISEMI

Ufafanuzi wa Takwimu kwa ufupi
Mkoa wa Lindi una jumla ya maeneo ya utawala yanayojumuisha mamlaka za miji na wilaya. Katika mamlaka za miji, Manispaa ya Lindi ndiyo mji pekee, yenye kata 31, mitaa 117, vijiji 47, na vitongoji 236.

Kwa upande wa mamlaka za wilaya, kuna wilaya tano: Mtama, Kilwa, Ruangwa, Liwale, na Nachingwea. Jumla ya maeneo haya ya wilaya ina kata 121, vijiji 476, na vitongoji 2,166. Hii inafanya mkoa mzima wa Lindi kuwa na jumla ya kata 152, mitaa 117, vijiji 523, na vitongoji 2,402.

SOMA PIA: Special Thread: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Majimbo ya Uchaguzi - Mkoa wa Lindi
Orodha kamili ya majimbo ya uchaguzi katika Mkoa wa Lindi, ikiwa na idadi ya kata na vitongoji, pamoja na Manispaa ya Lindi:
  1. Jimbo la Lindi Mjini (Manispaa ya Lindi)
    • Kata: 31
    • Vitongoji: 236
  2. Jimbo la Mtama (Wilaya ya Mtama)
    • Kata: 20
    • Vitongoji: 508
  3. Jimbo la Kilwa Kaskazini (Sehemu ya Wilaya ya Kilwa)
    • Kata: Sehemu ya kata 23 za Wilaya ya Kilwa
    • Vitongoji: Sehemu ya vitongoji 347 vya Wilaya ya Kilwa
  4. Jimbo la Kilwa Kusini (Sehemu ya Wilaya ya Kilwa)
    • Kata: Sehemu ya kata 23 za Wilaya ya Kilwa
    • Vitongoji: Sehemu ya vitongoji 347 vya Wilaya ya Kilwa
  5. Jimbo la Ruangwa (Wilaya ya Ruangwa)
    • Kata: 22
    • Vitongoji: 436
  6. Jimbo la Liwale (Wilaya ya Liwale)
    • Kata: 20
    • Vitongoji: 351
  7. Jimbo la Nachingwea (Wilaya ya Nachingwea)
    • Kata: 36
    • Vitongoji: 524
Kwa jumla, idadi ya kata na vitongoji kwa majimbo yote ya Mkoa wa Lindi, pamoja na Manispaa ya Lindi, ni:
  • Kata Jumla: 152
  • Vitongoji Jumla: 2,402
TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
- Kuelekea 2025 - LGE2024 - Waziri Mchengerwa: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Bara utafanyika 27 November, 2024

UPDATES
- Kuelekea 2025 - LGE2024 - CHADEMA yakabidhiwa Ilani ya Uchaguzi kutoka kwa AZAKI 300 nchini

- LGE2024 - ACT Wazalendo: Mawakala wa Vyama vya Siasa wanalazimishwa kwenda kuapa Halmashauri ambako ni mbali na maeneo wanayotoka

- Kuelekea 2025 - LGE2024 - Imekaaje ukurasa wa Tamisemi huko Twitter kueleza habari za Ilani ya CCM?

- LGE2024 - Waziri Mchengerwa atangaza tarehe ya kuchukua na kurudisha Fomu za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, siku zaongezwa

- LGE2024 - RC Zainab Telack Ahimiza Wananchi Kujiandikisha Ili Kupiga Kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

- LGE2024 - TAMISEMI hii maana yake nini? Kwa nini wakala aruke nafasi hapo kwenye Daftari?

- LGE2024 - CHADEMA: Uandikishaji wa Majina Uchaguzi Serikali za Mitaa una kasoro nyingi

- LGE2024 - Amos Makalla: Makalla: Tulipokuwa tunajiandaa na Uchaguzi wenzetu walikuwa kwenye Maandamano!

- LGE2024 - Lindi: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Mary Majaliwa wajiandikisha kwenye daftari la Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa

- LGE2024 - Isihaka Mchinjita: Katika baadhi ya maeneo wagombea wetu wametakiwa ili wapewe fomu ni lazima wapeleke vitambulisho vya uraia

- LGE2024 Nachingwea: Asilimia 99 ya wagombea waliowekwa na CHADEMA waenguliwa kwenye Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa

- LGE2024 - Mkurugenzi wa TAMISEMI: Waandishi wa habari msitumie neno "Kukatwa Wagombea", ni kinyume na kanuni za Uchaguzi

- LGE2024 Polisi wamkamata na kumuweka Lock up Steven Membe, Mwanachama wa CHADEMA, nyumbani kwao Rondo

- LGE2024 Wasimamizi wa vituo vya Uchaguzi 1,213 wapewa mafunzo na kula kiapo

- Kuelekea 2025 LGE2024 Lindi: CHADEMA yazungumza kukamatwa kwa Steven Membe

- LGE2024 - Abdallah Kambaya: CCM inahudumia Wananchi katika misingi ya sera

- LGE2024 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awataka wananchi wa Ruangwa kupiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa

- LGE2024 Idrisa Kweweta: Wananchi ikataeni CCM kwa vitendo Novemba 27, 2024

- LGE2024 Lindi: Katibu Tawala Mkoa (RAS) ahamasisha wananchi kujitokeza kwenda kupiga kura

- LGE2024 Lindi: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa apiga kura kwenye Uchaguzi wa serikali za mitaa

- LGE2024 - Lindi: Mama Salma Kikwete ajitokeza Kupiga Kura

- LGE2024 - Lindi: CCM na CUF wafungana Matokeo ya Uchaguzi Liwale, Uchaguzi kurudiwa

- LGE2024 - Wenyeviti na Wajumbe 1953 wa Manispaa wala kiapo cha Uadilifu baada ya kushinda Uchaguzi

- LGE2024 - Lindi: Zitto alalamika matokeo ya Kilwa Kusini kutotangazwa licha ya ACT kushinda baada ya kuzuiwa na Askari

TAARIFA ZA MIKOA MINGINE:
- LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

- LGE2024 - Special Thread: Hali ya Vituo vya Kujiandikisha kupiga Kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kwa Picha na Video

- LGE2024 - Uzi Maalum wa Kasoro na Rafu kwenye zoezi zima la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

- LGE2024 - Barwan Salum: Walemavu watolewe hofu na wahamasishwe kuwania nafasi za uongozi

- LGE2024 - CUF: Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa lilikuwa na dosari, tunashauri muda uongezwe

- LGE2024 - Amos Makalla: CHADEMA hawakuwa na kura za maoni kupata wagombea uchaguzi wa Serikali za Mitaa

- LGE2024 - Makalla: CCM hatuhitaji upendeleo wala kubebwa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, TAMISEMI itende haki

- LGE2024 - CCM: TAMISEMI itambue demokrasia yetu ni changa, ipuuze makosa madogomadogo katika hatua ya rufaa uchaguzi Serikali za mitaa

- LGE2024 - Makamu Mwenyekiti wa ACT Bara: CCM imekuwa ni genge la wahalifu. Kazi pekee wanayoweza ni kulipa rasilimali za umma!

- LGE2024 Lindi: Viongozi wa Dini na Kimila wasema uchaguzi umefanyika kwa Uhuru na Haki, Uchaguzi ujao amani itawale kama sasa

IDADI YA WATU WALIOJIANDIKISHA
- LGE2024 - News Alert: - Waziri Mchengerwa: Jumla ya wapiga kura milioni 31, 282,331 wamejiandikisha kupiga kura Uchaguzi Serikali za Mitaa 2024

MATOKEO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
- LIVE - LGE2024 - Matokeo ya Jumla Uchaguzi Serikali za Mitaa kutangazwa

- LGE2024 - Lindi: CCM na CUF wafungana Matokeo ya Uchaguzi Liwale, Uchaguzi kurudiwa

- LGE2024 - Lindi: CCM yashinda kwa asilimia 99.9 kwenye Wilaya ya Mtama
 
Back
Top Bottom