Pre GE2025 Lindi: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Pre GE2025 Lindi: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mada hii itakuwa na 'Updates' za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Lindi. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kushiriki na wengine.

1729433718290.jpeg

Ramani ya Mkoa wa Lindi

HISTORIA YA MKOA WA LINDI
Mwaka 1961 wakati Tanganyika inapata Uhuru wake kutoka kwa Waingereza Mkoa wa Lindi haukuwapo kabisa katika ramani. Kilichokuwapo wakati huo ni Jimbo la Kusini ambalo lilijumuisha Mikoa ya sasa ya Lindi Mtwara na Ruvuma. Makao Makuu ya Jimbo hilo la Kusini yalikuwa katika Mji wa Lindi. Hadhi ya Mji wa Lindi kuwa Makao Makuu iliishia mara baada ya Uhuru ambapo Jimbo la Kusini likawa linajulikana kama Mkoa wa Mtwara. Makao Makuu yakawa ni Mji wa Mtwara. Yamkini Mkoa wa Mtwara ulikuwa mkubwa sana kwa eneo hata Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Mtwara Bwana John Nzunda alikuwa anasema:

“Natawala kipande cha nchi toka Pwani ya Bahari ya Hindi hadi Ziwa Nyasa na kutoka Mto Ruvuma hadi karibu na mto Rufiji.” Serikali wa awamu ya kwanza Iliyoongozwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliugawa Mkoa wa Mtwara miaka ya mwanzo ya Uhuru ambapo kukawa na Mikoa ya Mtwara na Ruvuma. Mgawanyiko huu uliifanya Lindi kuwa ndani ya Mtwara.

Julai 1, 1971 ndipo Mkoa wa Lindi ulianzishwa rasmi baada ya tena kuugawa Mkoa wa Mtwara. Makao Makuu ya Mkoa yakawa Mji wa Lindi. Wakati Tanzania inaadhimisha Miaka 10 ya Uhuru wa Bara kwa kuwaita Waingereza kuja kuiona hatua iliyopiga Mkoa ulikuwa na umri wa miezi 6 tu.

HALI YA KISIASA
Mkoa wa Lindi una jumla ya majimbo nane (8) ambayo yote yana wabunge kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa mujibu wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

MAJIMBO YA MKOA WA LINDI
  • Jimbo la Kilwa Kusini​

  • Jimbo la Kilwa Kaskazini​

  • Jimbo la Mtama​

  • Jimbo la Lindi Mjini​

  • Jimbo la Mchinga​

  • Jimbo la Nachingwea​

  • Jimbo la Liwale​

  • Jimbo la Ruangwa​


UPDATES​

- Kuelekea 2025 - Gerson Msigwa: Serikali yawahakikishia wananchi Uchaguzi Huru na wa Haki 2025


MATUKIO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MTAA YA MKOA WA LINDI SOMA
- LGE2024 - Lindi: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024

- LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024


Januari
  1. Lindi: Wapiga kura wapya 121,187 watarajiwa kushiriki kwenye Uchaguzi mkuu mwaka 2025
  2. Lindi: Mkuu wa wilaya ya Nachingwea aboresha taarifa zake kwenye daftari la kudumu la mpiga kura
  3. Lindi: ACT Wazalendo walalamikia mchakato wa uandikishaji daftari la mpiga kura. Wasema hawajashirikishwa
  4. Lindi: Viongozi, Wananchi wajiandikisha daftari la mpiga kura, wahamasisha wananchi kujitokeza
Februari
  1. UVCCM Lindi: Vijana acheni kuwa madalali wa wagombea, wanaofanya kampeni kampeni kabla ya muda kukiona
  2. Mwenyekiti Halamshauri ya Wilaya ya Nachingwea: Rais Samia ameboresha maisha ya wananchi wa Nachingwea
  3. DC Nachingwea awaonya wahandisi miradi kujengwa chini ya kiwango
  4. Maimuna Pathan akabidhi milioni 2 kusaidia ujenzi wa nyumba ya mtumishi UWT na Mitungi ya Gesi 68 kwa Wakazi wa Liwale
Machi
  1. Lindi: Zaidi ya watu 120,000 wanufaika Samia Legal Aid
  2. Lindi: Mbunge wa Viti Maalum achangia bati 90 ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Nachingwea
  3. Wakili Mpanju: Wanawake mjitokeze kugombea nafasi za uongozi kwenye Uchaguzi Mkuu
  4. Salma Kikwete: Wanawake tusifanye ajizi, rafiki wa mwanamke ni mwanamke. Tupige kura za kihistoria kwa Rais Samia
  5. Mbunge Maimuna Pathan agawa mitungi ya gesi kwa wanawake wilaya ya Liwale
  6. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa Milioni 4 kwa wanafunzi wa Nachingwea Girls
  7. Waziri Mkuu, Majaliwa agawa mitungi ya gesi kwa wanawake 3000 kuhamasisha nishati safi
 

Attachments

Back
Top Bottom