LGE2024 Lindi: Mbunge wa Mchinga, Salma Kikwete ajiandikisha kwenye daftari la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

LGE2024 Lindi: Mbunge wa Mchinga, Salma Kikwete ajiandikisha kwenye daftari la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Mhe. Salma Rashid Kikwete, ameshiriki katika zoezi la uandikishaji wa wakazi lililofanyika kijijini Ruvu, kitongoji cha Makasini, kata ya Mchinga, Jimbo la Mchinga, mkoani Lindi.

Soma pia: Freeman Mbowe ajiandikisha Uchaguzi Serikali za Mitaa

Akizungumza na viongozi wa chama pamoja na wananchi wa kijiji cha Ruvu leo, tarehe 17 Oktoba 2024, baada ya kushiriki zoezi hilo, Mhe. Salma Kikwete aliwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la mkazi na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji, na vitongoji utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024.

Sk.png

Aidha, alitumia fursa hiyo kuwahimiza wanawake wa jimbo la Mchinga kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi zilizotangazwa kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji, na vitongoji.
 
Pamoja na kulipwa mafao ya mke wa Raisi mstaafu bado kakomaa tu na ubunge
Anakula pesa kila upande haachii wengine
 
Back
Top Bottom