Pre GE2025 Lindi: Mkuu wa wilaya ya Nachingwea aboresha taarifa zake kwenye daftari la kudumu la mpiga kura

Pre GE2025 Lindi: Mkuu wa wilaya ya Nachingwea aboresha taarifa zake kwenye daftari la kudumu la mpiga kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Leo tarehe 29 Januari 2025, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mhe. Mohamed Hassan Moyo, ameshiriki kikamilifu katika zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura.

Mhe. Moyo amewashauri wananchi waliofikia umri wa miaka 18 na wale ambao hawajajiandikisha, kujitokeza ili kujiandikisha. Pia, amewataka wale waliohamia maeneo mengine kuhakikisha wanahakiki taarifa zao. Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa kila mtu kutekeleza haki yake ya kupiga kura.

Zoezi hili limeanza tarehe 28 Januari hadi 3 Februari 2025, na ni fursa muhimu kwa kila mwananchi mwenye haki ya kupiga kura kuhakikisha taarifa zao zipo sahihi katika daftari la wapiga kura.

"Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora."


dc tabora.png
 
Back
Top Bottom