Lindi Mwambao watoa msaada wa Madawati, Viti vya Walemavu, na Matairi

Lindi Mwambao watoa msaada wa Madawati, Viti vya Walemavu, na Matairi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Chama Kikuu cha Ushirika cha Lindi Mwambao kimemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva madawati 150,viti mwendo 2 na mataili 4 kwaajili ya jeshi la Polisi, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 19,700,000 ikiwa ni kutekeleza msingi wa saba wa Ushirika wa kuisaidia jamii.

Hafla ya makabidhiano ya msaada huo imefanyika leo Novemba 20,2024 katika Ofisi za chama hicho zilizopo Mitwero kata ya Rasibula.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo,Mkuu huyo wa Wilaya ya Lindi ametumia fursa hiyo kuwaomba kuzidi kuwa walezi wazuri wa vyama vya msingi na kuifikia jamii kama msingi wa saba wa ushirika unavyotaka huku wakiendelea pia kutoa huduma bora kwa wakulima.

Meneja wa Lindi Mwambao Nurdin Said Swallah amesema wamezidi kusukumwa kwa namna Rais Dkt.Samia anavyojali ushirika kwa kusambaza pembejeo bure kwa wakulima hali iliyosaidia kuongeza uzalishaji wa korosho.
 
Back
Top Bottom