Lindi ni Mji Mkongwe Uliosahaulika

Lindi ni Mji Mkongwe Uliosahaulika

VANDYBLEAZE

Member
Joined
Dec 28, 2024
Posts
5
Reaction score
10
Ramadhan Mubarak

Baada ya kuimaliza mkoa wa pwani unaingia mkoa wa lindi kwa kuanza na wilaya ya kilwa

Safari ni ndefu kama masaa matatu hivi unaingia kwenye mji mkongwe, uliotawala amani na utulivu.

Upepo unasukumwa na mawimbi ya bahari ya hindi, tambarare na milima ya kuchosha mwili na kabila linaloongoza mji huu ni wamakonde na wamwela.

Hata ukikosa pa kulala kwenye mji huu wageni wake hawana hiyana utakaribishwa na kuishi nao kwa amani na ujamaa mutaunda.

Asilimia kubwa ya watu wa mji huu wanajishughulisha na shughuli za kilimo na uvuvi na wakitegemeana na wafanyakazi wa serikali ambao wanasubiri mishahara kila mwisho wa mwezi.

Kasoro za mji huu ni nyingi ila moja kubwa ni maendeleo hafifu, uchumi duni ukifika mkoa huu kupata fursa labda utafute kwa darubini kali. Wengi wa watu wa mji huu hawafanyi shughuli za kiuchumi ili wakue bali wanafanya shughuli za kiuchumi kwa ajili ya kukidhi matakwa ya matumbo yao tu.

Sijajua sababu za serikali kuufanya mkoa huu kuwa wa mwisho kimaendeleo licha ya rasilimali za kutosha kama gesi,bahari, ardhi ya kilimo na amani na utulivu...

KARIBU LINDI, PARIIIS!!
 
Kipindi hiki cha mama kuna fursa nyingi zimeletwa Lindi, kama Ujenzi wa kampasi tofautitofauti za vyuo, mradi wa gas asilia Mtimkavu na vitu/mambo vingine kama hivyo.. HAKIKA Lindi ni Mji wa kula bata tu ndogondogo bila kusahau samaki, pweza.
Kusini kuchele, I love Lindi
 
Back
Top Bottom