Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mkuu wa TAKUKURU (M) LINDI Mhandisi Abnery J. Mganga akitoa taarifa kwa umma kuhusu kuwafikisha mahakamani wafanyabiashara watatu (3) ambao ni:
1. Bw. Abdallah Said Luyaya, Mfanyabiashara na mmiliki wa duka la pembejeo liitwalo LUYAYA KILIMO KWANZA lililopo Wilaya ya Nachingwea
2. Bw. Ismail Fakihi Tebwa, Mfanyabiashara na mmiliki wa duka la TEBWA AGRO DEALER lililopo Wilaya ya Nachingwea
3. Bi. Jasmine Julius Mwalami, Mfanyabiashara na mmiliki wa duka la JASMINE AGROVET lililopo Wilaya ya Ruangwa Kwa tuhuma za kuingiza nchini na kuuza viuatilifu (pesticides) aina ya SELECRON 720 EC 500ML ambavyo vimepigwa marufuku kutumika nchini.
Watuhumiwa hao wamefikishwa leo hii katika Mahakama ya Wilaya Nachingwea na Mahakama ya Wilaya ya Ruangwa, ili kujibu tuhuma zinazowakabili baada ya uchunguzi kukamilika na kupata kibali kutoka Ofisi ya Mashtaka cha kuwafikisha hao mahakamani.