Pre GE2025 Lindi: Zaidi ya watu 120,000 wanufaika Samia Legal Aid

Pre GE2025 Lindi: Zaidi ya watu 120,000 wanufaika Samia Legal Aid

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Kamati ya msaada wa Kisheria imewasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli hiyo iliyodumu kwa muda wa siku 10 ndani ya mkoa wa Lindi tangu ilipozinduliwa Februari 19, 2025 wilyani Ruangwa na Mhe. Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kampeni hiyo imefanya kazi katika Halmashauri zote za Mkoa wa Lindi ikiwa imezifikia kata 74, vijiji 163, Mitaa 59 na kufanya jumla ya mitaa na vijiji 222.

Kampeni ilijikita katika kutoa huduma ya elimu ya Masuala ya kisheria , haki za binadamu na utawala bora, haki za watu wenye mahitaji maalum, Ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto, Ndoa,Mirathi na Wosia, Ardhi, Ajira na Mahusiano kazini.

Mratibu wa kampeni hiyo Mkoa wa Lindi Daudi Murumbe amesema zoezi la kutoa msaada wa kisheria Mkoani Lindi limefanyika kwa mafanikio kwani jumla ya Wananchi 121,483 walifikiwa na huduma, huku Wanaume wakiwa 55,462 na Wanawake 66,021.

Daudi ameeleza ipo migogoro ambayo iliweza kutatuliwa papo kwa papo na mingine iliendelea kushughulikiwa. Ametoa shukrani kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi , Katibu Tawala Mkoa na kamati ya maandalizi kwa ushirikiano ambao umesaidia kukamilisha zoezi hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amepongeza utaratibu huo ambao umeleta mafanikio katika mkoa wa lindi , amewasihii kuweka misingi imara ambayo itasaidia wananchi kuendelea kupata huduma hiyo kwa urahisi.

Soma pia: Pre GE2025 - Kampeni ya Samia Legal Aid yatua mkoani Lindi kutatua changamoto za wananchi za kisheria
 
Familia ya mzee Ali Kibao haijafanikiwa kufikiwa na hii huduma?
 
Back
Top Bottom