Linex: Nilipigiwa simu na Dj Khaleed nikachanganyikiwa.

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Msanii Wa Muziki wa Kizazi kipya anayefanya vizuri hivi sasa na Mkwaju wake mpya 'Got me' Sunday 'Linex' Mjeda amefunguka na kudai kuwa wiki mbili zilizopita alipokea simu ya Msanii na Dj Maarufu Wa Marekani Dj Khaleed.



Akizungumza na IdrisKitaa kupitia kipindi cha Twenzetu cha Times Fm, Linex amedai baada ya kupokea simu ya Dj Khaleed ambaye kwa wakati huo alikuwa mjini California, alichanganyikiwa asijue cha kufanya hali iliyomfanya Dj Huyo baba Wa Mtoto mmoja akate simu.

"NilimDm tu kwenye Instagram nikawa naisifia album yake kwamba ni Kali, nikaandika mambo mengi na kumtaka kama atataka kolabo na Msanii Wa Afrika nipo tayari" Alisema.

"So niliandika vitu vingi tu, asubuhi naamka nashangaa simu yangu inaita namba za nje afu imeandika California, ile kupokea Whats up, na sauti ni ya Dj Khaleed ile nashangaa akakata simu" Aliongeza.

Katika hatua nyingine Linex amesema amejaribu kumpigia Mara kadhaa lakini simu haipokelewi tena.

Chanzo: Times FM
 
Aisee hata mimi nilicomment kwa Trump kule twitter, nikamwambia kama atahitaji waziri toka afrika anipigie tu, sasa jana usiku wakati nimelala akanipigia bwana sema simu ilikua kwenye silent, sikuisikia naamka nakuta 5 missed calls from Trump.
 
Najua kuchanganyikiwa kwa furaha kupo lkni bwana linex angejikaza kiume akaongea ajue anasema nini maana kitendo cha kupigia simu Dj Khaleed ni sawa na kuokota dhahabu bombani.Aiseeh.
 
[emoji23][emoji23][emoji23].ananikumbusha kuna chuo cha carolina.nilitaka kujiunga na kozi za online sasa nikaweka namba zangu.si wakanipigia bhana.dada anaongea huyooo.hata simwelewi.nikakata simu.akapiga tena sijapokea.na juzi kanipigia tena.sijapokeaa

Sent from my TECNO-Y4 using JamiiForums mobile app
 
pole bhana,kisicho riziki hakiliki.

Sent from my TECNO M3 using JamiiForums mobile app
 
huyo jamaa ni mwongo sana msimuamini hata kidogo,namfahamu kwa ukaribu jinsi anavyopenda kick za kidwanzi hana jipya lolote huyo jamaa,,,kaona hasikiki kaamua aje na staili hiyo ili hako kanyimbo kake uchwara kasikilizwe,hawa ndio wanafanyage nimheshimu sana yule mzee aliyebarikiwa na kauli yake ya ELIMU,ELIMU,ELIMU!
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mkuu mbona unapishana na lamentali
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mkuu mbona unapishana na lamentali
Yule dada
Anaongea balaa namba zao hizo hapo

Sent from my TECNO-Y4 using JamiiForums mobile app
 
Ooouugghhhh... Dj khaleed.? okay

Sent from my GT-N7105 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…