Lini utekaji wa watu kupitia watu wasiojulikana utakoma?

Lini utekaji wa watu kupitia watu wasiojulikana utakoma?

Utawala2025

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2023
Posts
1,144
Reaction score
2,755
Habari.

Kama kila siku vyombo vya dola vinatuhamasisha wananchi tuweze kulinda Amani ya nchi Yetu.

Lakini Hali hii kwa hivi karibuni nchini mwetu imekuwa kitu cha tofauti na kuleta sitofahamu kwa sisi wananchi.

Kumekuwa na wimbi kubwa la wananchi kutekwa kwa vipindi tofauti na mazingira yasioeleweka huku taarifa nyingi zinazotolewa katika mitandao ya kijamii kwa kusema watu wasiojulikana.

Hali hii imeendelea kuleta taharuki kwetu sisi wananchi na kutuacha maswali na sitofahamu.

Kwanini mpaka leo Serikali kupitia Raisi wa nchi,Bunge la Tanzania ,mahakama ,Jeshi la polisi nchini Tanzania kukaa kimya na kutotoa tamko kwa hali ya utekaji inayoendelea nchini.

Je, ukimya wao unaleta picha ipi kwetu?

Ni kifanyike kama wao wameshindwa je wanataka tuwe frontline wa kupinga na kukemea vikali hali inayoendelea nchini mwetu.

Kwanini watu wachache wameamua kuwa juu ya sheria.

Naomba nimalizie kwa kutoa mifano miwili iliyotokea kwa kipindi cha miezi miwili na hatujaona matamko yoyote.

1. Utekaji wa SATIVA ni nani ametoa Tamko hadi leo?

2. Utekaji wa kijana shadrack Chaula maarufu kuchana picha ya Raisi nchini Mamlaka gani imetoa Tamko hadi muda.

Je, lini tutarajie kukoma utekaji nchini Tanzania?

PIA SOMA
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
 
Utaisha pale Kila mtu atafanya mambo yake pasipokuingilia mambo ya mtu mwinginee...

Niongezee sauti au inatoshaa
 
Tumuulize Rais Samia maana yupo kimya kuhusu itekaji as if wanaotekwa ni raia wa Burundi.
 
Ni pale tutakapo amua kama Taifa kwamba siasa isiwe KAZI ya malipo makubwa kama ya ualimu n.k!ndipo mauaji,rushwa,kupotezana,uhasama,mauaji ya ualbino na n.k vitakoma!

Mataifa yaliyoendelea siasa siyo kazi inayolipa sana Bali uweledi mbali mbali ndio hulipa Hulu kwetu ni tofauti ndio maana Kuna ujinga mwingi kuliko uerevu!!

Wenye mamlaka waamue vizuri kuhusu hiki ninachokiandika!
 
Ni pale tutakapo amua kama Taifa kwamba siasa isiwe KAZI ya malipo makubwa kama ya ualimu n.k!ndipo mauaji,rushwa,kupotezana,uhasama,mauaji ya ualbino na n.k vitakoma...
Aisee nimeona hii hata Kenya.

Mbunge analipwa million 7 halfu wanaishi maisha ya kawaida sana njoo bongo Miungu watu tu.

Angalia USA biden kirahisi tu anaachia uraisi njoo kwetu
 
Huta wasikia CCM wakizungumzia au kulaani suala la utekaji linalotokea nchini, kitu ambacho kinaashiria kuwa suala hill liko mikononi mwao na ili utekaji uishe ni mpaka CCM yenyewe itakapotekwa na kupelekwa mahali pasipojulikana.
 
Habari.

Kama kila siku vyombo vya dola vinatuhamasisha wananchi tuweze kulinda Amani ya nchi Yetu.

Lakini Hali hii kwa hivi karibuni nchini mwetu imekuwa kitu cha tofauti na kuleta sitofahamu kwa sisi wananchi...
Halafu nimekuwa nilikuuliza, hivi Jeshi la Polisi na TISS Wana maslahi gani hasa kwenye suala hili la utekaji Watu?

Kwa nini muda wote wamekuwa wapo kimya kabisa wakati zinapoibuka shutuma za kuwatuhumu wao kuhusika na vitendo hivyo viovu vya utekaji Watu?

Ukimya wao kwenye masuala haya huwa unamaanisha Nini hasa? Endapo kama kweli wao wamekuwa hawahusiki na matukio hayo ya utekaji Watu.

Je, ni kwa nini huwa hawachukui hatua zozote zile kali ili kujisafisha kutohusika na tuhuma kama hizo wanazotuhumiwa nazo?
 
HIVI NI KWANINI KWA SASA HII SIASA NA DEMOKRASIA YA NYAKATI HII MTU WAKIONA ANAITETEA ANAPOTEZWA WEWE KAMA MWANA JAMII UNALIONAJE. HILI TUPE MAONI
 
Utaisha pale Kila mtu atafanya mambo yake pasipokuingilia mambo ya mtu mwinginee...

Niongezee sauti au inatoshaa
Ukishakua kiongozi wa JMT Hilo sio Jambo lako. Ni Jambo la watanzania wote. Huwezi kukaa madarakani ukafanya uxenge ukasema ni Jambo lako hupaswi kuingiliwa. Utakua mpumbavu wa mwisho. Achia madaraka kafanye Jambo lako chumbani na mke wako. Akikukosoa mteke yeye na wanae.
 
Habari.

Kama kila siku vyombo vya dola vinatuhamasisha wananchi tuweze kulinda Amani ya nchi Yetu.

Lakini Hali hii kwa hivi karibuni nchini mwetu imekuwa kitu cha tofauti na kuleta sitofahamu kwa sisi wananchi.

Kumekuwa na wimbi kubwa la wananchi kutekwa kwa vipindi tofauti na mazingira yasioeleweka huku taarifa nyingi zinazotolewa katika mitandao ya kijamii kwa kusema watu wasiojulikana.

Hali hii imeendelea kuleta taharuki kwetu sisi wananchi na kutuacha maswali na sitofahamu.

Kwanini mpaka leo Serikali kupitia Raisi wa nchi,Bunge la Tanzania ,mahakama ,Jeshi la polisi nchini Tanzania kukaa kimya na kutotoa tamko kwa hali ya utekaji inayoendelea nchini.

Je, ukimya wao unaleta picha ipi kwetu?

Ni kifanyike kama wao wameshindwa je wanataka tuwe frontline wa kupinga na kukemea vikali hali inayoendelea nchini mwetu.

Kwanini watu wachache wameamua kuwa juu ya sheria.

Naomba nimalizie kwa kutoa mifano miwili iliyotokea kwa kipindi cha miezi miwili na hatujaona matamko yoyote.

1. Utekaji wa SATIVA ni nani ametoa Tamko hadi leo?

2. Utekaji wa kijana shadrack Chaula maarufu kuchana picha ya Raisi nchini Mamlaka gani imetoa Tamko hadi muda.

Je, lini tutarajie kukoma utekaji nchini Tanzania?

PIA SOMA
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
Utekaji hauwezi kukoma wenyewe bila ya kukomeshwa.
 
Back
Top Bottom