Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Nchi yetu ilipopata uhuru mwaka 1961 ilikuwa ni nchi ya vyama vingi mpaka mwaka 1965 Nyerere alipoamua kuifanya nchi ya chama kimoja kwa takribani miongo mitatu. Hatimaye vyama vingi vilirejeshwa tena mwaka 1992 pasipo ridhaa ya wananchi walio wengi.
Mwaka 1964 Uliundwa muungano tulio nao mpaka leo pasipo maoni au ridhaa kutoka kwa kundi lolote la wananchi pande zote za muungano. Kila tukihoji tunaambiwa huu ni urithi wetu na tunu yetu tukiwa hatujui hasa urithi huu na tunu ilipatikanaje.
Katiba yetu ya mwaka 1977 ni katiba isiyotakana na maoni ya wananchi na pamoja na matobo mengi yasiyofaa hata kuweka viraka tena tunaambiwa inatutosha na hakuna haja ya kushona vazi jipya wa tufanye mambo mengine ya maendeleo.
Ni wakati sasa wa wananchi wa Tanzania wachukue fursa ya kuamua mustakbali wao na kuijenga nchi yao wenyewe badala ya kuachia kikundi kikundi kidogo cha watu wanaoamini kwamba waemkuwa wanajua mahitaji ya watanzania milioni 60 mpaka sasa kwa miaka 60.
Siku njema yaja ambayo walio wengi wataamua mustakbali wa nchi yao wenyewe. Siku hiyo ni pale walio wengi si tu watakaposema imetosha bali watakapoweza kujipanga"organize" na kushirikiana kimkakati kuleta mabadiliko.
Sehemu yoyote duniani ukiona watu wamaefanikiwa kwa chanya au hasi ni kwa sababu waliweza kutengeneza ushirikianao imara. Chama cha kikomunisti cha China kina wanachama milioni 91 tu lakini kmefanikiwa kutawala nchi ya watu bilioni 1 na milioni 300 tangu mwaka 1949 kwa sababu ya ushirikianao imara.
Vyama vingi vya ukombozi vya Africa kama KANU vilikufa pale viliposhindwa kuendelea kuwa na ushirikianao ndani yake na miongoni mwa makundi mengine katika jamii.
CCM imedumu miaka mingi madarakani kwa sababu ya ushirikiana ndani yake na kwa makundi mengine muhimu ya kijamii kama dini, wafanyabiashara na wasanii, na vyombo vya habari na pia kuweza kumaliza migogoro ndani yake.
Njia pekee ya kuleta mabadiliko ni kwa ushirikiano mpana wa wanaotaka hayo mabadiliko.