Freyzem
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 10,120
- 24,667
Nyota wa soka nchini Argentina Lionel Messi amemuoa mpenziwe wa utotoni nyumbani kwao katika kile kilichotajwa kuwa harusi ya karne.
Waliokuwa wachezaji wa barcelona Xavi na mkewe, Fabregas na Mkewe na Chrales Puyol
Sherehe hiyo kati ya Messi mwenye umri wa miaka 30 na Antonela Rocuzzo mwenye umri wa miaka 29 ilifanyika katika hoteli ya kifahari katika mji wa Rosario.
Nyota wa soka na watu maarufu walikuwa miongoni mwa wageni 260 huku mamia ya maafisa wa polisi wakipelekwa kushika doria.
Kiungo wa Argentina Lavezzi
Messi na Rocuzzo walikutana wakiwa watoto wa miaka 13 kabla ya yeye kuelekea Uhispania.
Miongoni mwa wageni katika harusi hiyo ya Ijumaa ni wachezaji wenza Luis Suarez, Neymar, Gerrard Pique na mkewe Nyota wa muziki Shakira.
Idadi kubwa ya wageni walisafiri kuelekea Rosario katika ndege za kibinafsi.
Hali ilivyokuwa katika hoteli ya Rossario
Gazeti la Argentina la Clarine limeitaja harusi hiyo kuwa harusi ya mwaka na harusi ya karne.
Source: BBC