Lionel Mess afunga ndoa na mpenzi wake wa utotoni.

Freyzem

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2013
Posts
10,120
Reaction score
24,667

Nyota wa soka nchini Argentina Lionel Messi amemuoa mpenziwe wa utotoni nyumbani kwao katika kile kilichotajwa kuwa harusi ya karne.


Waliokuwa wachezaji wa barcelona Xavi na mkewe, Fabregas na Mkewe na Chrales Puyol

Sherehe hiyo kati ya Messi mwenye umri wa miaka 30 na Antonela Rocuzzo mwenye umri wa miaka 29 ilifanyika katika hoteli ya kifahari katika mji wa Rosario.

Nyota wa soka na watu maarufu walikuwa miongoni mwa wageni 260 huku mamia ya maafisa wa polisi wakipelekwa kushika doria.



Kiungo wa Argentina Lavezzi

Messi na Rocuzzo walikutana wakiwa watoto wa miaka 13 kabla ya yeye kuelekea Uhispania.





Miongoni mwa wageni katika harusi hiyo ya Ijumaa ni wachezaji wenza Luis Suarez, Neymar, Gerrard Pique na mkewe Nyota wa muziki Shakira.

Idadi kubwa ya wageni walisafiri kuelekea Rosario katika ndege za kibinafsi.



Hali ilivyokuwa katika hoteli ya Rossario

Gazeti la Argentina la Clarine limeitaja harusi hiyo kuwa harusi ya mwaka na harusi ya karne.
Source: BBC
 
Reactions: PNC
duuh sijuh kale kademu nilikuwa nafukuzia miaka hiyo kakowapi jamani...
 
Hatars mbona cwaoni aisee,,,naona wamepotezana kinoma
 
Reactions: PNC
Mwenzangu na mimi unakutana mjini na mwanamke baada ya miezi mitatu unatangaza ndoa. Akikubadilikia ndani ya nyumba unaanza kulalamika siku hizi hakuna mapenzi ya kweli.
 
Reactions: PNC
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…