Lionel Messi ametangaza rasmi kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Argentina

Papillon 1906

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
228
Reaction score
753
​

Lionel Messi ametangaza rasmi kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Argentina. Taarifa hiyo ameitoa leo, Agosti 31, 2026, kupitia ujumbe kwenye Instagram yake.

Messi amesema amefikia uamuzi huo baada ya kutafakari kwa muda mrefu tangu fainali ya Kombe la Dunia 2026, akieleza kuwa ni uamuzi unaomuumiza lakini anaamini “ni wakati sahihi.” Pia amesema kizazi kipya cha wachezaji kinastahili kupata nafasi.

Soma Pia: Neymar Jr atangaza kustaafu kuichezea Brazil baada ya kuondoshwa Kombe la Dunia na Norway

Maumivu ni makubwa sana, na itachukua muda kuweza kulifunga jeraha hili. Lakini pia ninabaki na kila jambo jema tulilopitia… Pamoja na michezo tuliyogeuza matokeo kwa kupambana hadi dakika ya mwisho, ambayo itabaki milele katika kumbukumbu, pamoja na uungwaji mkono wa taifa zima ambao, ukiunganishwa na kazi na juhudi za kundi hili, ulitufanya kwa mara nyingine tena tufike miongoni mwa timu bora zaidi duniani.

Leo ni vigumu kutambua thamani ya kile tulichokifanya, lakini kundi hili lilifika katika fainali mbili mfululizo za Kombe la Dunia.

Asanteni sana kutoka moyoni kwa kila salamu na kila ujumbe. Kwa mara nyingine tena, tuliweza kuungana kama taifa na kuwa pamoja, tukishirikiana katika fahari kubwa ya kuwa Waargentina.

Rekodi zake za Timu ya Taifa


2006-2026

Mechi alizo cheza - 207
Magoli - 125
Passi za magoli - 68

Mataji
1. world cup (2022)
2. coppa America (2021,2024)
3. Finalissma (2024)

True legend
=============


Your browser is not able to display this video.
 
Ameshatangaza kusitaafu tangu mwaka 2016 huko nyuma lakini akaendelea kuichezea timu yake ya Taifa, hivyo si ajabu tukimuona kombe la Dunia lijalo
 
Zama zao, (Ronaldo, Messi), zimeshakwisha. Kombe la dunia 2026 ni kielelezo tosha kwao. Mpira ni muda.
 
Hatimaye leo Messi ametangaza kustaafu kuitumikia timu yake ya taifa ya Argentina.

Ikumbukwe kuwa hii ni mara ya pili kutangaza kustaafu soka la Taifa.

Kila la heri GOAT
 
Ronaldo bado hataki kuamini kuwa nyakati huja na kuondoka
Baada ya kutolewa kwenye WC, Ronaldo alitangaza kuwa ile ndio mechi yake ya mwisho kuitumikia Portugal.

Nchi yake ikamuomba asistaafu maana potential yake kwa nchi ni kubwa.

Ronaldo mpaka saizi hajatupa comment yake kuhusu maoni hayo kutoka kwa viongozi wake wa nchi.
 
Argentina bila ya fifa wataishije? mana hapa kuna dalili za kuwaacha mkono tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…