Lionel messi: kuna haja ya kujikana wewe mwenyewe...

Lionel messi: kuna haja ya kujikana wewe mwenyewe...

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
15,966
Reaction score
26,404
Mara nyingi mwanadamu anaishi mara moja tuu.. ndiyo! ni moja tuu...

alizaliwa pale Argentina.. akatua nchini hispania akiwa na miaka kumi!...na tena akiwa na matatizo changu nzima.. lakini Barcelona waliona kipaji chake! Akafanyiwa matibabu ya kila namna.. na hatimaye aliyoyafanya yanajulikana... sio mwingine ni Lionel Andres Messi..
mchezaji mwenye mafanikio. ila taifa lake linamuangusha!....
Messi huko alipo moyoni anajuta.. Anajuta kwanini hakuchagua team ya Spain??.. Messi sio muargentina! Messi ni muhispaniola aliyekulia kwenye misingi ya kikatarunya!..
kwake Messi kuhama Barça ni tusi kubwa kwa wakatarunya!..
Kafundishwa zaidi misingi ya Barcelona kuliko Argentina!. angeweza kucheza Spain Kama sio ushauri wa baba yake Jorge Messi.. Wakati kwa mara ya kwanza anaenda kambi team ya Argentina!... watu walidhani ni kijana wa kihispaniola.. mpole, mwenye lafudhi ya kihispaniola, mkimya... ni muargentina wa kurithi ila muhispaniola wa damu.... leo hii wenzake aliocheza nao Barça akina Iniesta wana medali ya kombe la dunia.. ukiachana na kombe la dunia lenyewe!...
kwa sasa anacheza na kina Gonzalo higuan!, ambao wakiwa kwa club zao wanafanya vizuri... ila wakienda team ya taifa.. mzigo anaachiwa Messi!.. wanajua hata wakifungwa lawama atapewa Messi....
pole Lionel Messi... kwa yaliyokutokea.. ni mpuuzi pekee atawaangalia kina Di Maria wakiwa na uzi wa Argentina!...
Messi anajuta kwanini alisikiliza akili yake badala ya kuufata moyo wake!...
"mwanadamu anaishi Mara moja "...

"mchizi kichizi "..
 
Messi mzalendo na ana misimamo yake na sio lazima uwepo kwenye kikosi cha wachezaji bora ili ushinde vikombe, umesahau Argentina walivyo fika fainali ya kombe la Dunia Brazil 2014?
Hayo yoteeee kama umesoma utaelewa mkuu..
 
Messi ni mzalendo...narudia tena Messi sio mhispaniola bali ni Muargentina asili. Najivunia sana kuwa mzalendo....kukosa w/c sio ishu...so atabakia kuwa mfalme/mchezaji bora kuwahi kutokea katika ulimwengu wa soka
 
Messi ni mzalendo...narudia tena Messi sio mhispaniola bali ni Muargentina asili. Najivunia sana kuwa mzalendo....kukosa w/c sio ishu...so atabakia kuwa mfalme/mchezaji bora kuwahi kutokea katika ulimwengu wa soka
Sikupingi mkuu..
 
Messi na Christian Ronaldo japo hawana/hawajabeba kombe la dunia bado watabaki kuwa wachezaji bora kuwahi kutokea kwenye ulimwengu wa soka.
 
Back
Top Bottom