Lipa namba imekuwa kero sana

quadrupleA

New Member
Joined
Apr 16, 2021
Posts
3
Reaction score
5
Wadau Mimi ni mfanyabihashara ya Tigo pesa na Mpesa, nimekuja kugundua ghafla commission imeshuka, na kugundua kwamba binti niliye muweka dukani ana line ya lipa namba ya Tigo, so mteja akija kutoa pesa ana mshawishi atumie lipa namba na akitoa mfano elfu 99000 anakata 1500 yake cash.

Mkononi mteja anabaki na balansi baada ya kukatwa hiyo 1500 na msichana ambayo ni ndogo kwa mteja ukilinganisha na tozo ambayo angekatwa kama angetoa kwa wakala direct.so mie nabaki sina kitu? Nifanyeje?
 
Fukuza kazi huyo yupo kwa masilahi yake binafsi,hivyo mwisho wa siku utakua unatoa pesa ya pango mfukoni mwako na sio kwenye biashara.
 
Natafta suruhisho...ugawaji waline za lipa namba mamlaka ziangalie tena.....hakutakiwa na haja ya kufanya bihashara ya kutoa pesa lasivyo hii kwangu kesho kwa mwingine..
 
Natafta suruhisho...ugawaji waline za lipa namba mamlaka ziangalie tena.....hakutakiwa na haja ya kufanya bihashara ya kutoa pesa lasivyo hii kwangu kesho kwa mwingine..
Hii huduma nlikuwa nataka kufanya mipango ya kujiunga lakini naona kunapoelekea hizi kusagiana kunguni mda sio mrefu itawekewa vikwazo hii huduma ngoja nitulie tu
 
Mkuuu naona unataka tukale police????
 
Mkuu pole toa tu hio namba ya lipa
 
Yani mfanyakazi ana biashara yake ndani ya biashara yako na inaathiri mapato yako,Lakini hujui cha kufanya!?
 
Hii shoti ya umeme uliyopigwa, imetokana na hili tangazo lako, au kuna sababu nyingine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…