Lipi jema


Swtheart,
  1. Hebu watafsiri wanisaidie tofauti ya ku SHOW na ku EXPRESS love... maana kuna observable na non-observable emotional expressions, kwenye mapenzi utawezaje 'kuonyesha' non-observables?

Tatizo linalotukumba wengi, tunaogopa sana vivuli vyetu na jamii inavyotu judge, mfano huo kama kulaumiwa kwa kupenda 'sana!'.
Kupenda ni kupenda tu, hakuna mwanzo wala mwisho, hakuna kiwango wala kipimo, ...mapenzi yana 'uhai', yanakuwa, yanadhurika, na yanakufa na mengine hufufuka!. Mapenzi ni mapenzi...ukipendwa mshukuru kweli Mungu kwani kuna wengine hawajabahatika bado kupendwa.

Bahati mbaya, si lazima yule unayempenda naye anakupenda kama utavyotaka akupende. Oohhh,...I can go on, and on and on...bora tu niishie hapa, maana moyo wangu unaungua kwa mapenzi...
 
swala la kupenda linatokea automatically na huwezi kulicontrol,na ndio maana huwezi kuamua kuonyesha au kutokuonyesha hisia hiyo,itakuja tu na utashangaa hata mama yako anakwambia, 'i know you are in love...'


...BAK, salama kaka...za masiku? ha ha ha...
nakubaliana nawe na 'daughter' hapo juu 100%...
Kitufe cha Thanks sikioni... lakini michango yenu inastahili "thanks"
 
...BAK, salama kaka...za masiku? ha ha ha...
nakubaliana nawe na 'daughter' hapo juu 100%...
Kitufe cha Thanks sikioni... lakini michango yenu inastahili "thanks"

Salama Kaka, nafurahi kukuona maana nilikuwa karibu kuanzisha thread ya kukutafuta baada ya kutokukuona kwa kipindi...kumbe nikagundua tunapishana mitaa tunayotembelea.....Jamii forum kubwa ati lol! Kitufe kipo bro hebu nigongee basi hiyo kitu nijinome hahahahahaha.
 

...bht, ...LOL,....tupo wengi wa aina yako. Yaani moyo ulishavunjwa vipande vipande sasa vimeungwa ungwa tu kwa supa glu. Wanaosema wanapenda kwa kiasi nadhani wanamaanisha wanapenda kwa tahadhari. Ndio wale utaowasikia 'weshaumwa na nyoka' wakiona unyasi haooo... Lakini ya nini kupenda mguu ndani mguu nje kama unaibia bana?

All in all, sidhani kama ni sahihi makosa ya aliyekuwa Ex-wako ndio iwe life sentence. Yaani yakufanye uishi maisha ya wahka na wasiwasi tele.
Utajinyima furaha bure ilhali maisha yenyewe mafupi haya. Kuna waliona uwezo wa kukusahaulisha majeraha yote yaliyopita, ila kuondoa makovu ya mapenzi rohoni ni jukumu lako wewe uliyejeruhiwa. Usipofanya hivyo ndio utaishia kila siku "...unanitonesha bana, usiniguse hapo..!"
 
Hivi UPENDO na MAPENZI ni vitu viwili tofauti?? Naomba kujua
 
Hivi UPENDO na MAPENZI ni vitu viwili tofauti?? Naomba kujua
TOFAUTI SANA mkuu!upendo ndo muhimili wa NDOA!

mapenzi NI kitu cha kawaida kwenye levo ya ''ngono'' katika kurefresh tu....!unaweza ngonoa na mtu kwa maana ya mapenzi tu AU KWA MAPENZI YAKO TU!...halafu huyo mtu akawa nje kabisa na kitu ''PENDO'' moyoni mwako ''baba askofu''

ukiona mume/mke anatoka nje ni ni kwa ajili ya mapenzi tu na kutimiza ''haja za kimwili''!lakini UPENDO!...HUU NI UGONJWA WA TAIFA!KAMA MATHEMATICS MASHULENI
 

Mbu we acha tu!!! mtu unajisemesha eti I will never love again........but its not out of ur own will that u fall in love!!!

healing process ya majeraha ya mapenzi ni ngumu sana kwa kweli ila ukijibidisha unapona na maisha yaendelee. one doesnt have to deprive him/herself of love life.

nadhani ukimpata mtu mkapendana maisha ni mazuri sana!!

so I wont hesitate expressing /showing love kwa yule ntakayempenda kwa woga wa kuumizwa
 
Dada yangu dont put that sad look on your face. Hukufanya vibaya kumuonyesha mtu unampenda. Its worth at the time. Ila yeye ndo wa ajabu kukulipizia kwa chuki badala ya mapendo
thanks JS, unajua watu wengi tunachanganya mtu kujitolea kwa mwenza na unyonge... Na its even worse kama jamaa ana inferiority complex. BTW, hivi kumuonyesha mtu mapenzi sana ndio kumpa sanaa? Au kumlea sana?
 
thanks JS, unajua watu wengi tunachanganya mtu kujitolea kwa mwenza na unyonge... Na its even worse kama jamaa ana inferiority complex. BTW, hivi kumuonyesha mtu mapenzi sana ndio kumpa sanaa? Au kumlea sana?
hapo utanidai bia tatu!...please!umeongea kitu fulani OUTSTANDING
 
Ngumu!! Kupenda huwa kunakuja bila mwenyewe kujua.. Unajikuta umependa balaa! Pole MJone! Dawa kama unaweza, Usijaribu kuingia kwenye huo mchezo wa KUPENDA.. Ni MATATIZO.
 

Once again thank you bht, mimi pia nimewahi kuumizwa kimapenzi kutokana na umbali tu tena ndani ya Tanzania yetu. Tulipendana sana na ilikuwa ni raha tupu lakini kuhamia mkoa mwingine ikawa sababu ya kuharibika kwa penzi letu lakini najua raha ya kupenda na kupendwa na kamwe sioni sababu ya kuficha mapenzi yangu ya kweli kwa yule nimpendaye eti kwa kuogopwa kuumizwa.
 
penzi ni kikohozi.. (I mean true love) huwezi kulificha ....
 
Kwa kweli mmenifungua sana macho yangu katika huu ulimwengu wa mapenzi. So huwa ni hadithi za kijiweni tu kuwa ... usimwonyeshe mwanamke kuwa umempenda sana ....atakutawala eh?
 
Kwa kweli mmenifungua sana macho yangu katika huu ulimwengu wa mapenzi. So huwa ni hadithi za kijiweni tu kuwa ... usimwonyeshe mwanamke kuwa umempenda sana ....atakutawala eh?

MJ1 mimi sikubaliani na dhana hiyo na wala sijawahi kutawaliwa katika idara hii. Sidhani kama ni hadithi za kijiweni tu kuna watu wanaamini hivyo. Ukimuonyesha kwamba unampenda sana basi ataanza "kukuzingua" au "ataleta za kuleta"
 
MJ1 mimi sikubaliani na dhana hiyo na wala sijawahi kutawaliwa katika idara hii. Sidhani kama ni hadithi za kijiweni tu kuna watu wanaamini hivyo. Ukimuonyesha kwamba unampenda sana basi ataanza "kukuzingua" au "ataleta za kuleta"

Aise hii imenigusa sana...this is how my hubby does, alafu cha ajabu all his friends says oooh, jamaa anakupenda sana, mara anawivu sana na wewe...nikiangalia naona kama vile wanayosema niuongo. Imenipelekea all my love which i had for him kupotea kabisaaaaaa. Siku hizi namuacha aendel zake popote anapotaka...cha ajabu sasa ndo ameanza kuonyosha kujali, wivu, kupenda etc. Yoooote ya nini haya, watu wengine watakujaga poteza bahati zao hivi kwa kitu eti kutokuumizwa kimapenzi. 😡
 

kweli sometimes bahati inahitajika
 
nimeshaumizwa sana yaani huu umoyo ulishavunjika mpaka there are no more pieces to break.

What??? nipe AK47 yangu.....haya niambie ni wakina nani wamehusika!!

lakini ina maana umekuwa hard-core!!
 

Poor you! Umeamua kukubali mitala siyo?
 
Jamani mnasahau kitu kimoja kuna kupenda na kutamani hivi vitu viwili ni tofauti kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…