umeoa/umeolewa ushauri , mawazo au maelekezo yapi ni ya kuya fuata? Unayopewa na mmeo/mkeo au wazazi? Na kama mwenzi wako anafuata sana yale anayopewa na wazazi kulioko ya mmewe/mkewe je yupo sasa hihi? Na kama hayupo sahihi wewe kama mme/mke ufanyeje?
Naomba mawazo yenu wana jf!!!!!!!!!
kila mtu atakupa maelekezo lakini wewe unatakiwa utumie akili yako kuya changanua...
uchukue yale tu unayojua unayahitaji nayatakusaidia hayajalishi nanani kayasema......
Sawa lakini ikatokea kwa asilimia 90 unafuata unayoambiwa na wazazi si ina maana mmeo/mkeo hana haja ya kuwa naye na pia kila analokuambia mmeo/mkeo kuhusu hayo mawazo uliyotoa kwa wazazi huambiliki unashikilia hayo hayo, kweli hii ni ndoa sahihi?