Lipuli yamtoa kwasi kwa million 25

Ekyoma

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
2,177
Reaction score
2,804
LIPULI YAMTOA KWASI KWA TSH. MILIONI 25

Uongozi wa klabu ya Lipuli FC inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara umeridhia maombi ya klabu ya Simba ya kumsajili beki wake raia wa Ghana, Asante Kwasi, kwa ada ya uhamisho ya shiilingi milioni 25.

Taarifa iliyotolewa na idara ya habari na mahusiano ya Lipuli FC imeeleza kuwa tayari Simba imekamilisha taratibu zote za usajili zinazohitajika na hivyo kuanzia sasa Asante Kwasi ni mchezaji halali wa Simba SC.

“Uongozi wa Lipuli FC unakiri kupokea barua yenye ombi la kumtaka mchezaji tajwa hapo juu na kwa kauli moja umeridhia kumaliza sintofahamu hiyo kwa kumruhusu mchezaji Asante Kwasi kwenda Simba SC kwa ada ya uhamisho ya kiasi cha shilingi milioni 25,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
 
Fowadi muhimu sana muda huu simba ikicheza kwani jana walitia aibu
 
Namaanisha ilikuwa bora km angesajiliwa fowadi
Mnae mavugo,Gyan,Bocco,Okwi hadi Niyonzima anacheza mbele mnataka nini tena!!
Kuna mpya anaitwa Domingo na yule mzambia sijui mtawaweka wp nao.
 
Sasa wafunge dirisha la usajili maana lengo lao limetimia.
Ingekuwa Yanga ndiyo watasajili wakati huu, Hatakuja angekuwa anaharisha maneno
 
Mnae mavugo,Gyan,Bocco,Okwi hadi Niyonzima anacheza mbele mnataka nini tena!!
Kuna mpya anaitwa Domingo na yule mzambia sijui mtawaweka wp nao.
Jamaa wamechanganyìkiwa kila mchezaji wanamtaka. Ni ngumu sana kwa kocha wa simba kufanyakazi na uongozi wa simba ndo mana mayanja alijiondoa mapema
 
Hizo 25 ndiyo rasmi. Wajanja wameishapiga za kwao. Mo anaibiwa mchana kweupe
 
Tayari ameshasajiliwa!!! Eti system ya usajiri imeshatengemaa
Je, ni halali kwa waumini wahusika kula kitoweo cha mnyama aliyetangulia kufa na baadaye ndio akachinjwa?Je, Simba walikuwa na haki ya kumsajili Kwasi wakati taratibu zenyewe za usajili wa mchezaji huyo walikwishazivunja?Je, makubaliano ya Simba na Lipuli yanafuta kosa la Simba kuzungumza, kumficha na kuingia mkataba na Kwasi wakati akiwa ndani ya mkataba na Lipuli? Je, yanaivua ile jezi ya Simba aliyoivaa Kwasi mazoezini wakati akiwa bado ni mchezaji halali wa Lipuli? Je, yanafuta hoja ya ile barua ya malalamiko kwa TFF dhidi ya Simba kuhusu jambo hilo? Je, Yanga watarejeshewa 50,000,000/- walizotozwa kwa kosa kama hili kuhusiana na Hassan Kessi, ingawa yeye tayari alikwishafungiwa na timu yake kwa muda mrefu zaidi ya ule wa kumalizia mkataba wake? Je, kanuni za Ligi na za Soka zinaweza kuvunjwa iwapo timu mbili zitaridhiana kutozifuata, mathalan Lipuli kuridhia goli la kuotea watalofungwa na Simba hata kama mwamuzi atalikataa; au TFF kutoichukulia hatua Yanga dhidi ya Mbao iwapo itamchezesha mchezaji asiyesajiliwa madhali Mbao yenyewe haikukata rufaa? Nilidhani ubabaishaji wa aina hii ndani ya TFF ni historia, kumbe ndio uhalisia! Halafu tunashangaa Tanzania kuporomoka kwa viwango vya FIFA!
 
Jamaa wamechanganyìkiwa kila mchezaji wanamtaka. Ni ngumu sana kwa kocha wa simba kufanyakazi na uongozi wa simba ndo mana mayanja alijiondoa mapema
Mayanja hakujiondoa brother, hawa viongozi wetu wanatimua hawa watu kwa kuwatengenezea mambo mambo tu.
 
Sasa wafunge dirisha la usajili maana lengo lao limetimia.
Ingekuwa Yanga ndiyo watasajili wakati huu, Hatakuja angekuwa anaharisha maneno
Malinzi aliwabeba sana nyie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…