CUF Habari
JF-Expert Member
- Dec 12, 2019
- 239
- 234
BUKOBA MJINI
Nitahakikisha kuwa Bajeti ya Wizara ya Afya inapanda na kufikia asilimia 15 ya
Bajeti ndani ya miaka 10 ijayo. Ongezeko la bajeti litawezesha katika kuandaa miundombinu ya kisasa, wataalam, vifaa tiba na vipimo vya kutosha kwa
maradhi yote.
Aidha ongezeko la bajeti litawezesha kutenga fungu maalum kwa ajili ya kukabili maradhi ya milipuko kama COVID-19 kwa kadri yatakavyojitokeza. Ili kuhakikisha kuwa kila raia ana haki na anapata
huduma za msingi za afya, Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itahakikisha asilimia 70 ya Watanzania wote wana Bima ya Afya ifikapo 2025 na asilimia 100 ifikapo 2028.
Hatua maalumu zitachukuliwa kuhakikisha
kuwa huduma za uzazi bila malipo zinapatikana kwa kila mama mjamzito ili
kupunguza vifo vingi vinavyotokea ambavyo vinadhibitika.
"Hii miaka mitano hali ya maisha ilivyokuwa ngumu, vijana wa Katoro mmetubadilishia msemo mnasema vyuma vimekaza, sasa ndugu zangu mwenye glisi (Grease) ya kulegeza hivyo vyuma vilivyokaza ni Prof.Ibrahim Haruna Lipumba"
"Hali ya umasikini inazidi, mzunguko wa fedha unazidi kupungua, vijana wa Katoro mnazeeka kabla ya wakati wenu". Prof Ibrahim Lipumba