- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, amesema Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe amemzuia kwenda katika ofisi kutokana na yeye kueleza ubadhirifu unaofanywa ndani ya chama.
Pia Lissu amesema sababu nyingine ya kuzuiwa kwenda katika ofisi hizo ni kutokana na kutoa siri za vikao ndani ya chama, na kumueleza ukweli kuhusu kitendo cha kuanzisha taasisi nyingine ndani ya CHADEMA.
Aidha Mwanahalisi ina nakala rasmi ya barua ya siri ambayo Mbowe amemwandikia Lissu kwa kumpiga zuio la kwenda ofisini.
Pia Lissu amesema sababu nyingine ya kuzuiwa kwenda katika ofisi hizo ni kutokana na kutoa siri za vikao ndani ya chama, na kumueleza ukweli kuhusu kitendo cha kuanzisha taasisi nyingine ndani ya CHADEMA.
Aidha Mwanahalisi ina nakala rasmi ya barua ya siri ambayo Mbowe amemwandikia Lissu kwa kumpiga zuio la kwenda ofisini.
- Tunachokijua
- Tundu Lissu ni Mwanasheria ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema lakini pia aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Singida mashariki mwaka 2010 hadi mwaka 2020
Kupitia kipindi cha Dakika 45, cha ITV Agosti 26, 2024 Lissu akielezea uhusiano wake na mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe aliwahi kusema uhusiano wake na Mwenyekiti ni mzuri na hawajawahi kugombana lakini kupo kutofautiana kwa misimamo ya kisiasa akisema kuwa ni jambo la kawaida kutokana na kuwa wao ni watu wawili wenye mitazamo tofauti, na watu hutumia mwanya huo kukuza mambo na kuonesha kama kuna mgogoro baina yao.
Mapema leo, Septemba 7, 2024, kumekuwa na taarifa ambayo imekuwa ikisambaa mtandaoni ikimtaja makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu kuwa amekiri kuzuiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kwenda ofisini kutokana na kueleza ubadhirifu unaofanywa ndani ya chama hicho.
Sehemu ilipochapishwa taarifa hiyo ni hapa, hapa na hapa.
Ukweli wa jambo hili upoje?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini Lissu hajazungumza maneno haya.
Mathalani, kwa kutumia Keyword Search ("Amemzuia kwenda katika ofisi") kama sehemu ya maneno yanayopatikana kwenye ujumbe huo, JamiiCheck haikupata ushahidi muhimu unaoelekea kwenye kurasa rasmi za Mwanahalisi, CHADEMA, Lissu mwenyewe, mtu au chombo chochote cha habari cha kuaminika.
Kwa kutumia Google Reverse Image Search, JamiiCheck imebaini kuwa ujumbe huu haujawahi kuchapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya Mwanahalisi Digital kama inavyodaiwa kwani hakuna kumbukumbu rasmi zinazoonesha historia ya ujumbe huo kuwahi kuchapishwa mtandaoni na ukurasa huo.
Kwa kurejea mpangilio wa utengenezaji wa Graphics zinazotumiwa na ukurasa wa Mwanahalisi digital, JamiiCheck imegundua mapungufu kadhaa ya Graphic inayosambaza uzushi huo ikiwemo kukosekana kwa mstari mweupe unaotenganisha sehemu ya juu ya maneno ‘Mwanahalisi Digital” na sehemu ya chini unapoandikwa ujumbe wa picha husika. Pia, Aina ya mwandiko (fonts) unaotumiwa na gazeti la mwanahalisi ni tofauti na ule unaoonekana kwenye ujumbe unaosambazwa mtandaoni.
Aidha, Septemba 7, 2024, muda mfupi baada ya kusambaa kwa taarifa hii, Kurasa rasmi za Mwanahalisi zilikanusha kuhusika nayo, na kuwaomba watu waipuuze kwani ilianzishwa na watu wenye nia ovu ili kufanikisha malengo yao binafsi.
Pia, Chanzo chetu cha kuaminika kimethibitisha kuwa Lissu karibu wiki ya 3 hayupo ndani ya nchi, na hivyo kutupa uhakika zaidi juu ya uzushi wa taarifa ya Lissu kufukuzwa au kuzuiwa kuingi ofisini na Mbowe.