Lissu alikuwa mwongeaji sana na Media akiwa Makamu Mwenyekiti, baada ya kupata Uenyekiti kimyaa

Shotocan

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2023
Posts
6,650
Reaction score
12,711
Lissu alikuwa mwongeaji sana na Media akiwa makamu mwenyrkiti ,baada ya kupata uenyekiti kimyaa. Uenyekiti sio lelemama alidhani lelemama.

Kuna taarifa za ndani kuwa alichokikuta baada ya kukabidhiwa kiti hakuamini macho yake.

Kabla kushika kiti aliaminishwa kuwa Chadema ina wanachama milioni nane kumbe ilikuwa propaganda tu kufika ofisini kakuta takwimu zinaonyesha wako laki nne na waliolipia ada za mwaka ni elfu 2 tu ambao ndio wanachama hai wa Chadema.

Kwenye kikao cha makabidhiano kilichofanyika hotelini Bagamoyo Lissu aligoma katakata kuongea na waandishi wa habari akidai hicho ni kikao cha kazi hakihitaji waandishi wa habari tofauti na tabia yake alikuwa nayo akiwa makamu mwenyekiti ya kupenda media kila akiwepo ziwepo kuwa yeye anapenda uwazi wa chochote cha chama sababu chama ni cha wananchi sasa hivi kaanza kukimbia media.
 
Amekuta mambo ni mbombongavu
 
Kuwa mwenyekiti wa chama pinzani katika nchi ya kidikteta iliyojaa UCHAWA na kulamba viatu vya watawala ni kazi kweli kweli inahitaji moyo
 
Unaposema uongo wa wazi kama huu sisi tunaojua ukweli tunabaki kukudharau tu.
 
Chawa kazini
 
Alichokuwa anapigania ameshakipata
 
Kwa hiyo Mbowe hakufanya lolote kuinua chama?
 
Hakuna kiongozi wa jumuiya yoyote halali Tanzania aliye kinyume na utawala. Nililisema hili hata kwa Mwambukusi.

Uongozi ni dhamana kubwa na ngumu sana kuitendea kazi, sababu mifumo inasomana na ndio uzuri wetu.
 
Kwa hiyo Mbowe hakufanya lolote kuinua chama?
Kazi ya kuinua chama ni ya kila kiongozi

Mbowe kanda ya kaskazini alikiinua sana Chama hadi ikainekana Chadema ngome yake Kaskazini iko vizuri

Lisu akiwa makamu mwenyekiti kanda yake mbona Chadema hamna kitu ? Alitaka Mbowe ndie aende kuhangaika kanda yake wakati yeye ndie makamu mwenyekiti?
 
najua, namaanisha hata mwezi haujaisha tangu awe m/kiti
sasa wewe unaposema haongei na waandishi wakati hana hata mwezi 1 unashangaza
Kikao alichofanya bagamoyo cha makabidhiano kwa nini aligoma kuongea na waandishi wa habari wakati yeye ndie mpinga usiri kwenye vitu vya chama akiwa makamu mwenyekiti? Anaficha nini kwani wakati akiwa makamu alisema mambo ya chama huhitaji uwazi hakuna cha kuficha wala siri ya kikao cha chama

Vyote vinatakiwa kuwekwa hadharani

Haya twende kazi ya kikao cha bagamoyo mbona kaufyata ?
 
Kwa hiyo kabla hajawa mwenyekiti alikuwa hajui idadi ya wanachama wakati alikuwa makamu mwenyekiti? Au unaumia Lissu kukabidhiwa ofisi na sio Mbowe? Hata kama atakuta huko ofisini mwanachama hai ni yeye peke yake furaha yetu ni kuona Mbowe na team yake waliotawala miongo 2 plus wameondoka basi. Hayo mengine tumuachie yule mkulima wa bamia kule kijijini Mbutu Block E.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…