- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu
Lissu alisema sababu ya wao kuzuiliwa kuingia Angola ni kwa sababu walihisiwa wana M-pox?
Lissu alisema sababu ya wao kuzuiliwa kuingia Angola ni kwa sababu walihisiwa wana M-pox?
- Tunachokijua
- Tundu Lissu ni Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Madai
Ipo grafiki inayosambaa mitandaoni ikifanana na zinazotumika na kurasa za mitandao za gazeti la Mwananchi (Mwananchi news), grafiki hiyo ikiwa na ujumbe kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Tunsdu Lissu anaeleza kuwa sababu ya wao kuziliwa Angola, ni kuwa walihisi viongozi hao akiwemo yeye wana Ugonjwa wa M-Pox. Tazama hapa na hapa.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia uhalisia wa madai hayo na kubaini kuwa hayana ukweli. Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao ikiwemo google image reverse na utafutaji wa maneno muhimu (Key word Search) tumebaini kuwa hakuna taarifa hiyo na haijachapishwa na Mwananchi News kama inavyoonekana.
Ufuatiliaji umebaini kuwa grafiki iliyotumika imeharirirwa kutoka kwenye grafiki ya Mwananchi News iliyotumika Februari 15,2025 wakati Lissu akizungumza na wananchi wa Manyoni akiwa anaelekea Ikungi Singida. Katika grafiki halisi Mwananchi News waliandika kuwa “Lissu: Nimejiandaa kufungwa katika kudai haki mfumo wa uchaguzi” Tofauti na grafiki iliyohaririwa na kutumika machi 17, 2025.
Aidha katika Taarifa yake aliyoitoa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X kuhusiana na sakata hilo, Lissu hakugusia suala la M-Pox kama sababu ya wao kuziliwa kuingia nchini Angola.
Pia hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na chama chake kueleza kuwa M-Pox ndiyo ilikuwa sababu ya wao kuzuiliwa kuingia nchini humo ambapo walieleza hakukuwa na sababu za msingi zilizotolewa za wao kuzuiliwa kuingia. Tazama hapa na hapa kuona taarifa zilizotolewa na CHADEMA kuhusu suala hilo.