Tundu Lissu ni Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa ambaye pia ametangaza nia ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika January, 2025.
Tangu Lissu alipotangaza nia ya kugombea nafasi hiyo dhidi ya Mwenyekiti anayemaliza muda wake ambaye naye pia ni mgombea wa nafasi hiyo
Freeman Mbowe kumekuwepo na mivutano mikali baina ya wafuasi wa viongozi hao na wakati mwingine pia baina yao wenyewe wagombea kupitia mahojiano mbalimbali wanayokuwa wakiyafanya kwenye vyombo mbalimbali vya habari na majukwaa mengine. Tazama
hapa,
hapa,
hapa na
hapa
Tarehe 31/12/2024 kumeibuka barua ambayo imekuwa ikisambazwa katika mitandao ya kijamii ikieleza kuwa siku ya jumatatu ya tarehe 6/01/2025 kamati kuu ya CHADEMA itafanya kikao maalumu kwa ajili ya kumjadili Lissu ambaye ni Makamu mwenyekiti kwa kuvujisha taarifa za ndani ya chama na kutoa kauli na tuhuma za uongo zinazotolewa mitandaoni dhidi ya viongozi mbalimbali wa chama.
Uhalisia wa barua hiyo upoje?
JamiiCheck imefanya ufuatiliaji kuhusu barua hiyo iliyowasilishwa na mdau wa JamiiCheck.com akihitaji kupata uhlisia wake ikiwa na grafiki ya TBC digitial inayomilikiwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na kubaini kuwa taarifa hiyo
si ya kweli na
haijatolewa na TBC digital.
JamiiCheck imefanya ufuatiliaji wa kimtandao na kubaini kuwa taarifa ama barua hiyo haijachapishwa katika kurasa za mitandao za
TBC digital kama inavyoonekana kwenye grafiki hiyo. Lakini pia ufuatiliaji wa kimtandao katika kurasa za
mitandao ya kijamii ya CHADEMA tumebaini kutokuwepo kwa barua wala taarifa kuhusiana na kuwepo kwa kikao hiko na kwa siku ya leo 31/12/2024 CHADEMA wamechapisha taarifa kuhusu kuachiwa huru kwa George Sanga na wenzake ambapo wameandika katika ukurasa wao wa X;
“Leo Desemba 31, 2024 Mahakama Kuu - Njombe imewaachia huru George Sanga na wenzake baada kukaa gerezani kwa siku 1555 kwa tuhuma za mauaji.” Tazama hapa na hapa
Aidha tumefuatilia katika
ukurasa wa mtandao wa X zamani ikijulikana kama Twitter wa Katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika ambaye pia katika kurasa zake hajaandika wala kuchapisha barua hiyo.
Mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano na mambo ya nje wa CHADEMA Jon Mrema kupitia ukurasa wake wa X amekanusha taarifa hiyo na kuwataka wananchi waiipuuzie kwa kuwa ni uzushi. Tazama
hapa