KWA NINI FAM TONGE ^LIMEMNYANG'ANYWA^?
1. Corruption scandal
2. Muda wa mabadiliko umebisha hodi
3. Poor combination ya Mbowe na Wenje.
Mbali na corruption scandal, Wenje alipwaya sana kwenye hiyo nafasi. Hana uzoefu wa kimawasiliano. Anapaniki haraka. Anajibu kwa kuridhika (anakosa passion yake binafsi, tofauti na wagombea wengine). Anajibu kwa mashaka na kujichanganya mwenyewe. Hana analosimamia na kutetea. Haoni mbele, bali anahofia mbeleni.
Hajui kabisa kupangua hoja na kujichotea pwenti hata kama amekuwa implicated kwenye kashfa fulani. Kwa mfano, TAL aliulizwa kwa nini hakuwajibika kujiuzulu baada ya kuhusika kumpitisha mgombea Wenje ambaye wakati huohuo anamtuhumu kuwa ana viashiria vya rushwa? (Hoja nzito na yenye mashiko kabisa)!
Lakini mstari mmoja tu wa TAL ulitosha kuwashawishi wajumbe kukubaliana naye: ^Mimi siwezi kuwajibika kwa madhambi ya mtu mwingine!^ Japo kimsingi hakujibu swali aliloulizwa, lakini kwa kauli hiyo na msisitizo uliofuata, tayari alikuwa amechukua pointi 3 muhimu!
Kwa upande mwingine, Wenje kila akijaribu kujibu ndipo anaharibu sana. Mbaya zaidi, hasikilizi hoja na kuikata kwa sentensi ya kwanza wakati akiijibu. Mzungumzaji anapojibu hoja fulani, lazima sentensi ya kwanza iwe dhahiri shahiri kiasi cha kujibu kwa muhtasari utata wote ulioibuliwa. Kauli zinazofuata ni kama ufafanuzi tu. Sanaa hii TAL na FAM wameimudu barabara!
4. Matarajio hewa. FAM na wapambe waliingia uwanjani na ushindi wao. Kuna shabiki mmoja aliahidi wangepanda ushindi wa zaidi ya 90%!!! Huku ni kujiamini kupitiliza - ambako bila shaka kuliwafanya wajumbe wa kati (ambao wako kotekote) waamue kuegemea kwa TAL - kulikosababisha anguko lake mwishowe.
5. 20 + 1 years!!! If you know, you know! According to TAL: Mitano tena italeta kitu gani kipya?
6. PPP - percentage of personal purity. Wengi wajumbe walimwona FAM kama mostly Sisiemu kuliko CDM, wakati TAL, kama alivyosema mwenyewe, msimamo wake unajulikana kwa wote.
7. Sera sintofahamu na utendaji usioridhisha: suala tata la maridhiano, matumizi ya fedha za chama, hatua (gani?) zilizochukuliwa katika chaguzi za nyuma zinazoaminiwa kuporwa, uimarishaji wa chama hasa hivi karibuni, chama kujiendesha yenyewe, suala zito na nyeti la Katiba Mpya na athari yake kuhusu uchaguzi mkuu ujao, nk.
8. Kihoja FAM<<<<<TAL. Unaweza kuthibitisha hili vizuri kabisa kwa hotuba ya hawa miamba wawili wakati wakiomba kura. Zingatia utamu na mvuto wa maneno (ufasaha) na hoja za msingi. Hotuba zote zimetulia kiufasaha na kimantiki, lakini kihoja na kiushawishi, mmoja anapwaya sana.
9. Timing. Wajumbe wanahoji: Nini hasa kilichomfanya FAM kugombea tena - maana ni kana kwamba alikuwa ameshaamua kukaa pembeni, halafu baadaye akashinikizwa (na nani?!), ndipo akaitisha ile press nyumbani kwake, akatangaza kuwachwana (challenge) wapinzani wake ^kwa boksi.^ Hofu hiyo ya wajumbe ikajitafsiri kwenye matokeo.
10. Busara na uelewa wa TAL. Wengi walitegemea, siku ya uchaguzi TAL angehamaki na kuwaparua na kuwararua kwa jazba wapinzani wake mbele ya wajumbe.
Lakini mambo yakawa kinyume chake. Kama ambavyo FAM alitulia tuli na kuvaa uungwana wote wa mwanakondoo, TAL naye akapita mulemule. Japo hakulegea kimsimamo, alijivika sura ya uvumilivu na kuahidi umoja na ushirikiano hata kama angeshindwa.
Nadhani hiyo ilimpa TAL pointi nyingi mno. Wengi walihofia angekihama CDM (kama Mchungaji PM). Lakini kauli yake ya kubaki CDM hata ingetokea akashindwa, na pia ahadi ya kuendeleza mapambano yake kwa ajili ya kujenga chama, viliwapa tumaini kubwa wajumbe na kuwafanya wamwone kama kinara asiyepaswa kupotezwa kamwe!
11. Uwazi katika upigaji kura.