Pre GE2025 Lissu apinga tuzo aliyopewa Samia na kusema kuwa huo haukuwa uamuzi wa Chama bali maamuzi binafsi ya Mwenyekiti, ataka ahojiwe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau hamjamboni nyote?

Jisomeeni wenyewe hapo chini kwa kiswahili

Jambo TV


Akizungumza kupitia mtandao wa Clubhouse usiku huu, Lissu ameeleza kuwa Rais Samia alialikwa na Mbowe kushiriki katika mkutano wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA), na walijulishwa tu kuwa mwaliko huo umetoka kwa Mwenyekiti.


Ameongeza kwa kusema kuwa, walishangaa kuona tuzo ikitolewa kwa Rais Samia bila kujulishwa mapema, huku kamati kuu ya chama hiyo ikiwa haijakaa kujadili suala hilo.


"Yalikuwa ni maamuzi ya Mwenyekiti pekee yake kwa haya mambo mawili. Hakuna kikao kilikaa kamati kuu kumwalika Rais Samia au kumpa tuzo," alisema Lissu, akimtaka Mwenyekiti Mbowe kuhojiwa kwa nini alitoa tuzo hiyo na kumleta Samia, wakati chama cha CCM kilikuwa hakijakubali chochote kuhusu maridhiano kati ya pande hizo.


Lissu amekumbusha kwamba masharti ya mwanzo ya maridhiano kati ya CHADEMA na Serikali yalikuwa na vipengele maalum, na kwamba anajiuliza ikiwa hatua ya kutoa tuzo kwa Rais Samia ni matokeo ya maridhiano hayo.?


Tuzo hiyo, aliyopewa Rais Samia Suluhu Hassan, ilitolewa na Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) mnamo Machi 08, 2023, kwa kumpongeza kwa juhudi zake za kuboresha na kuimarisha demokrasia nchini, huku akihusishwa na amani, upendo, na mshikamano.


Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwa Rais Samia na Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa niaba ya BAWACHA wakati wa Kongamano la Siku ya Wanawake lililofanyika mjini Moshi.
 
Bado unaamini huyu mtu anafaa kuwa mwenyekiti wa chama.

Predictable na wenzake wa clubhouse.
Kwa sababu huna akili ndiyo maana unaandika upuuzi huu. Hivi tuzo ilikua kwa ajili ya nini wakati watu wanauawa, watu wanatekwa na kupotezwa.

Mbumbumbu labisa wewe huwezi kumwelewa Lissu. Tuzo ni maamuzi ya vikao vya kamati kuu. Kama kamati kuu haikukaa, Mbowe alikubaliana na nani na kutoa tuzo kwa ajili ya nini?
 
Sasa mbona hakupinga wakati ule anangoja mpaka wakati wa uchaguzi? Mbowe atamgaragaza tu hata abwabwaje namna gani😁😁
 
Mimi najua sampuli ya wachangiaji wa clubhouse na uelewa wao
wa siasa.

Vita yangu ya siasa awahimudu, duh.
 
Hivi Jamaa wa hivi atakuwa asset au liability huko Chadema?

Chadema mchagueni huyu tuone Chadema itakuaje .

Nina uhakika Lisu akiwa Mwenyekiti wa Chadema ACT ndio itakuwa rasmi chama Kikuu Cha Upinzani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…