Pre GE2025 Lissu apinga tuzo aliyopewa Samia na kusema kuwa huo haukuwa uamuzi wa Chama bali maamuzi binafsi ya Mwenyekiti, ataka ahojiwe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mimi najua sampuli ya wachangiaji wa clubhouse na uelewa wao
wa siasa.

Vita yangu ya siasa awahimudu, duh.
Ni "hawaimudu" na sio " awahimudu".
Neno moja la kiswahili, tena la kawaida huwezi kuliandika, hiyo vita ya siasa utaiwezea wapi!!???
 
Ni "hawaimudu" na sio " awahimudu".
Neno moja la kiswahili, tena la kawaida huwezi kuliandika, hiyo vita ya siasa utaiwezea wapi!!???
Mimi nilishatoka huko uelewi somo tu. A/H sio kigezo cha akili.

Jenga hoja

Huna uwezo tulia pembeni.
 
Tuzo ilitolewa na BAWACHA si FAM. Hivi ninyi wagombea wa nafasi ya m/kiti Taifa Chadema ni shetani Gani anawavuruga Hivyo? Mimi ningependa mfanye UCHAGUZI wa kidemokrasia na isimamiwe na Watu wanaokubalika hasa wasio na masilahi na chama au TLS. Tupate matokeo sahihi Kwa kutumia sanduku la kura na si vinginevyo.
 
Mimi nilishatoka huko uelewi somo tu. A/H sio kigezo cha akili.

Jenga hoja

Huna uwezo tulia pembeni.
Makosa ya kisarufi na kifasihi yanayojirudia ni uthibitisho wa " slow learning".
Slow learning ni dalili moja ya ukilaza.
Naamini hili pia "uelewi" (huelewi).
 
Kwa nini Lisu hajuongea wakati huo ?

Lisu tapeli kubwa la kisiasa

Mbowe hatoki mitano tena kwa Mbowe
 
Mimi nilimshangaa sana Huyu mama kupewa tuzo wakati kafanya madudu mengi tu ambayo Kila mtanzania mwenye akili timamu anayajua
Na lissu kasema kwa sababu kaulizwa kuwa mlimpa tuzo kuheshimu kwa uwongozi uliotukuka asingeulizwa asingeleta hiyo hoja
 
ni upumbavu wa kiwango cha juu sana mlimwalika wenyewe mkampa na tuzo mnachoma vitenge ili iweje? mnaonekana mburula tu

..sio upumbavu.

..hao kina Mama wana sababu zao za msingi kuonyesha hisia zao kutokana na matendo mabaya ya Samia na serikali yake.

..moja ya hoja wanazozilalamikia ni utekaji, sasa huwezi kusema hoja hiyo ni upumbavu.
 
..hii hoja ni rahisi sana kuijibu.

..Mbowe anaweza kusema tuzo ililenga kumuonyesha Samia nia njema waliyokuwa nayo Chadema kuhusu maridhiano.


..Na kwamba tatizo sio yeye, bali Samia na Ccm ambao wamejibu matendo mema ya Chadema kwa ubaya.

..kuanza kumlaumu Lissu, na baadhi kumtukana, kana kwamba tunafurahia matunda ya maridhiano, na 4R, ni kutokujua kujibu hoja.
 
Nani kawafundisha ukorofi hawa ?
Nyerere na baba wa taifa hili alikikubali ichi chama kwamba kinaweza kuwa mbadala wa ccm , hatutakiwi kukichukia ,ila
Tuljivunie kuwa na chama ichi, mengine ni drama tu, au mapito tu , chama kitavuka salama asema Bwana
 
Akiwa yeye na nani? Maana maamuzi huwa yanatolewa na vikao vya kamati kuu kamati kuu haijatia baraka zake halafu unasema hoja nyepesi
 
Mbowe anatokaje kwenye tuhuma kama hizi? busara ilikuwa aache kugombea ampishe tundu lissu kunusuru chama
 
Akiwa yeye na nani? Maana maamuzi huwa yanatolewa na vikao vya kamati kuu kamati kuu haijatia baraka zake halafu unasema hoja nyepesi

..sidhani kama Mwenyekiti alikuwa na nia mbaya.

..Wabaya ni Samia na Ccm ambao wameitikia wema wa Chadema kwa ubaya.
 
..sidhani kama Mwenyekiti alikuwa na nia mbaya.

..Wabaya ni Samia na Ccm ambao wameitikia wema wa Chadema kwa ubaya.
Ndio maana sasa watu wanasema mwenyekiti bado ameganda kwenye siasa za kikwete wakati ccm uko haipo tena
 
Bado unaamini huyu mtu anafaa kuwa mwenyekiti wa chama.

Predictable na wenzake wa clubhouse.
Sasa wewe hapo unaona kipi cha kuuliza swali kama hilo. Hukuelewa maelezo yaliyo tolewa?

Au tuseme, kwa maana yako wewe, Mwenyekiti wa chama anayefaa kwa sifa unazo zijuwa wewe ni anaye shabihiana na huyo anaye elezwa katika taarifa hiyo iliyo andikwa hapo? Anaye jifanyia tu mambo bila kushirikisha viongozi wenzake?
 
..sidhani kama Mwenyekiti alikuwa na nia mbaya.

..Wabaya ni Samia na Ccm ambao wameitikia wema wa Chadema kwa ubaya.
Kwa hali iliyo jifunua hadi hapa tulipo fikia sasa, Mbowe hana tofauti yoyote na hao wa CCM. Ni mshiriki anaye juwa kinacho fanyika
 
Hivi Jamaa wa hivi atakuwa asset au liability huko Chadema?

Chadema mchagueni huyu tuone Chadema itakuaje .

Nina uhakika Lisu akiwa Mwenyekiti wa Chadema ACT ndio itakuwa rasmi chama Kikuu Cha Upinzani
Itabidi uongeze dua zako, Tundu Lissu aongoze CHADEMA; maana naona ndiyo unadhani itakuwa nafuu kwa huyo mnaye nyonya uchafu wake huko CCM.
Mnayo hofu kubwa sana kwa Tundu Lissu kuchukuwa uongozi wa chama.
 
Walau nimesikia alichoongea.

Lissu kwa sasa ni ‘now or never’ ni mfa maji.

Lakini ana hoja it must be said.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…