Uchaguzi 2020 Lissu asema atafuta vitambulisho vya machinga kwasababu elfu ishirini wanayotozwa ni wizi mtupu, haijulikani inaenda wapi

Mwanzo walikua wanatoa ushuru wa miatatu mpaka miatano kwa siku.bado na kipigo kutoka kwa mgambo na kuharibiwa mali zao ziliwahusu.
kwa sasa buku twenti kwa mwaka mzima tena bila bughdhwa ya mgambo.
Hapo ndo wamachinga ambao ni wengi watakapo muona Lissu ni zaidi ya adui kwa maisha yao.
 
Kuna Watu mnasema mleta mada anapotosha,na Wakati huohuo nyinyi hamsemi nini mwelekeo wa kauli ya mh Lisu

Nilisema hapa, Kuinanga hoja ya mh JPM kuhusu wamachinga bila kusema mbadala wake itakuwa hivi juu ya wamachinga ni kujichimbia shimo lefu sana

Ukweli kwa nini ufichwe? Sisi sote ni wajenzi wa Taifa letu, Lisu ni mjenzi wa Taifa letu, JPM na wengine wote ni wajenzi wa Tanzania

Na ndiyo maana, katka jukwaa hili,ziko hoja ambazo viongozi wetu huzichukua na kuzifanyia kazi na Taifa linapiga hatua

Ukweli ni kwamba, Wamachinga Pindi vitambulisho vyao vikiondolewa bila kuwa na mbadala wa hicho, ni bomu kubwa katika utawala wowote, kundi hili linawakilisha vijana wengi mno nchini

Ikumbukwe kipindi cha nyuma, police wetu kila Leo walikuwa wakiwindana na wamachinga kila uchwao, kama kusingepatikana dawa hii ya vitambulisho Hadi hivi leo, pengine kungekuwa na ugaribifu mkubwa maeneo mbalimbali ya miji yetu

Sasa, mh Lisu anaweza kulisema Hilo akiwa na lengo la kujiongezea wapiga kura na asijue bomu analoliunda kumhangaisha yeye Pindi awapo madarakani

Hivi vitambulisho vimewapa heshima na unafuu mkubwa wamachinga kwenye kufanya biashara zao, kero na kelele zile za kipindi cha nyuma hatuzioni tena

Sasa mpeni kichwa aingie mazima aje ajionee
 
Hayo umesema wewe hakuna pahali lisu kazungumzia elfu 20
 
Uongo hautakusaidia we dada,Mh Lissu amesema wazi kabisa vioe vitambulisho atavifuta na nina unga mkono maana ule ni mradi wa mtu vitambulisho vinatolewa ikulu hahahahha safari hii tutaelewa tu.
Wewe utakua ni mgambo uliyekuwa unanufaika na ukamataji wa machinga
 
Una makengeza ya kufikiri. Ukitoa urasmi hujui kama ndiyo unarudi kule kule kwenye kuwaumiza
 
Anataka kujua zinaenda wapi kwani ye ni serikali?
 
Mkuu unapotosha, amesema anafuta tozo ya machinga. Tena akaendelea kusema kama tozo hizo ni wizi mtupu.


Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
 
Wanaweza kuwa rasmi bila kulipa. Mbona tunao wanafunzi na hawalipi ada?
 
Nimemsikia kwa Maskio Yangu Hafai Kuwa Hata Mbunge
 
Hii ndio shida sasa.

Kwa dalili za mapema inaanza kuonyesha CCM watatumia muda mwingi kujibu/kupotosha hoja za Wapinzani kuliko wao kueneza zao. Kwa kiingereza watakuwa wanacheza Catch up game.
Hawana mpya tena, zile bombardier, stiglers... hamna mtu tena mwenye hamu nazo, miaka yote mitano walikuwa wakiimba.
 
Hawana mpya tena, zile bombardier, stiglers... hamna mtu tena mwenye hamu nazo, miaka yote mitano walikuwa wakiimba.
Hivyo ulivyovitaja vimetangazwa sana, kila mkutano, kila uzinduzi, kila semina, kila ziara, njiani akienda mikoa mbalimbali vilikuwa ni hivyo tu. Kumbuka hii mikusanyiko ilikuwa ni kila wiki.
Kuna wakati hata watoto wangu walikuwa wamecremisha idadi ya madarasa, hospitali na zahanati zilizojengwa, idadi ya fedha za mikopo, n.k

Rudi YouTube angalia mikutano ya miaka mi 4 iliyopita yote hotuba zinafanana.

Sasa Wananchi wanataka kusikia upande wa pili ya shilingi unasemaje?

Ili tujue hiyo October.
 
miundombinu inajengwa kwa hela za vitambulisho?
 
Mama, umbea siyo sifa nzuri. Tumia akili yako vizuri itakusaidia kuheshimika katika jamii na kuonekana ni binadamu kamili.

Kuendelea kuandika umbea kama huu, baadaye utazie na kugeuka kuwa ndiyo tabia yajo kuu katika jamii na hatimaye kupuuzwa na kudharaulika na kila mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…