Uchaguzi 2020 Lissu asema atafuta vitambulisho vya machinga kwasababu elfu ishirini wanayotozwa ni wizi mtupu, haijulikani inaenda wapi

Wala siku za machinga hazihesabiki sababu Tundulisu hawez kua Rais wa Tanzania

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Uongo hautakusaidia we dada,Mh Lissu amesema wazi kabisa vioe vitambulisho atavifuta na nina unga mkono maana ule ni mradi wa mtu vitambulisho vinatolewa ikulu hahahahha safari hii tutaelewa tu.
Watu wanaishi dunia ya mwaka 2000 kurudi nyuma huko, hicho kipindi tulikua tunategemea magazeti, radio na TV kupata habari, sasa hivi hata ITV ikidanganya, watu wanakuja na DATA kwamba hiyo habari mmedanganya, yaani sasa hivi mawasiliano yalivyo hayahitaji kua na reporter. Huyu mwandishi arudi shule akasome elimu ya kisasa, hiyo aliyonayo haitamsaidia kudanganya kwenye ulimwengu hu wa kisasa.
 
Mkuu wewe ni mpotoshaji wa kiwango cha kutisha! Ni nani asiyejua jinsi vitambulisho hivyo vilivoleta kadhia kwa wananchi wa mikoa ya pembezoni?? Wametozwa elf 20 hadi mafundi wanaoshona kandambili! Wametozwa 20,000 hadi mama ntilie na wenye maduka madogo ambao tayari walishalipa kodi na ushuru! Maeneo mengine walilazimishwa hadi walimu wavinunue hivyo vitambulisho wakati sio wajasiriamali na wanakatwa kodi kila mwezi! Mbaya zaidi mwanzo ilitangazwa kuwa ni hiayari ya mfanyabiashara lakini kadri muda ulivokwenda maagizo mazito yalizidi kutolewa toka juu na kuwatisha wakuu wa mikoa na wilaya kuwa asiyemaliza vitambulisho ameshindwa kazi! Matokeo yake wananchi ndio walioumia huku kukiwa hakuna sheria yoyote iliyotungwa na bunge kuhusu vitambulisho hivyo!
 
Heri wapatanishi maana watauona Ufalme wa Mbinguni.Kilichosemwa ni kufutwa hivyo vitambulisho,kuweka utaratibu rafiki hiyo biashara ifanyike vipi kwa kushirikisha na kuirasimisha bila kuharibu utaratibu wa biashara za wengine,kutoa fursa kwa vijana kupata ajira rasmi/zisizo rasmi badala ya uchuuzi huu.Pia hicho unachotaka kutuaminisha kitatokea kwa kubughudhiwa na Mgambo?Hao Mgambo ni Al shabab?Nani atawapa mamlaka ya Kukiuka Haki za Binadamu?Mh.Lissu na CDM kwa ujumla hawawezi kuruhusu matendo hayo ambayo waasisi wake ni CCM,siyo jukumu la Mgambo,Polisi ama Askari yeyote katika Jmhuri ya Muungano wa Tanzania aliye na haki ya kupiga Raia,hivyo ni baadhi ya vitu vitakavyobadilishwa Haraka sana CDM ikiingia Uongozini mnamo October 2020.
Twende Pamoja bila Hofu na Visasi(No Hate No Fear)
 
Mwanaume kabisa unajiita Rebeka. Shame
 
Misinformation to console yourself.
 
Kwamba hizo pesa zimetumika kujenga miundombinu ipi ? Sijaelewa maana duh.
 
Lisema kweli lipenzi la Mungu linazipiga elfu ishirini ishirini linazipelekwa kwao Rwanda.
 
Wanaweza kuwa rasmi bila kulipa. Mbona tunao wanafunzi na hawalipi ada?

Huko nyuma si kama vile hawakuwa wanalipa, nini kilichokuwa kinawatokea.? Ila sasa wakitaka kubughudhiwa unaambiwa waache hao nao wanachangia kodi. Ni wafanyabiashara rasmi.

Ndio maana tunawashauri machingaz na bodaboda wawe macho na Lissu, huu mzimu uliwalaghai cdm huko nyuma na kuwalisha uongo kuwa yeye na gege lake la cdm2015 ni wapigania haki. Kumbe, kuumbee, kumbe ni madalali wa kisiasa. EL alipokuja wakampangisha chama chao, fedha ya pango ati, aaatiii, ati, leo, leeoo, leo, hii Lissu huyuhyuuu, Lissu huyuhuyuu! Anawauliza wanacdm mliyaona mabilooni ya EL?!!! Huyu ni tapeli tu wa kisiasa.

Sasa, saaasaa,sasa! Mnisome, Machingaz na bodaboda wanao viongozi wao watumike kuwafikishia ujumbe wenzao wa kuwaelimisha wachukue tahadhari. Ule uhuni waliofanyiwa cdm 2015 safari machinfaz na bodaboda wamelengwa atawatumia. Wataachwa na kupigwa changa la macho baada ya oktoba 2020, mwenzao huo atatimkia huko alikokuweko.
 
Unajua ulichokiandika ni ujinga mtupu! Na kwa kujua hivyo ukaamua kuikimbia ID yako ya kila siku ili uweze kuandika hiki kituko. Pumba mwisho Lumumba siyo humu, humu utachapwa za uso tu.

 
Come 28 Oktoba
Chagua
Rais Chadema
Mbunge Chadema au ACT
Diwani Chadema au ACT
Usifanye makosa tena ya kuchagua matapeli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…