Tundu Lissu akizungumza na BBC Swahili kuelekea Uchaguzi wa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa uliofanyika Januari 21, kuhusu mabango na tofauti ya Kenya na Tanzania! ukweli mtupu akidai, "Somo kubwa la Kenya ni wamefikaje hapo walipo, ukisafiri kutoka Nairobi kuja Arusha ni Dunia mbili tofauti, kati ya Nairobi mpaka Nambanga na Nambanga mpaka Arusha"
"Ukitoka Nairobi mpaka Namanga alama unazoona barabarani mabango nini...biashara, uchumi watu wako kazini, kama ni mashamba ni mashamba kweli. Ukitoka Namanga (uhamiaji) na kuingia hivi (Tanzania) mamaa, mama, mama, mama. Picha njia nzima ni Mama, nyie hamna biashara yoyote ya kiuchumi, biashara yenu ya matangazo ni ya Mama!"
Tanzania tumefikia hatua hatari sana ya uchawa kiasi ambacho saivi hadi mambo ya msingi yanategemea uchawa.
Endapo CCM isipopumzika hii nchi ipo kwenye hatari kubwa sana ya kuanguka kwenye mikono watu hatari maana wameshaona siasa za hii nchi kupitia Chama cha Mapinduzi zimeshafikia hatua hatari sana ya kuzalisha na kutengeneza watu wa hovyo