Pre GE2025 Lissu calculated his moves

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

don-mike

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2011
Posts
600
Reaction score
1,178
kwa jicho la mbali naweza sema Lissu alipanga haya yanayotokea siku nyingi, pengine hata zaidi ya miezi 12 nyuma, na aliamua wapumbaza team Mbowe.

Kwa hali ilivyo sasa Team Mbowe wanacheza game ya Lissu. Siku BoniYai anatangaza vita hadharani, wenzake walikuwa wanamcheka pembeni kwamba kete zao zipo salama.

Kwa mtu aliyejiandaa muda mrefu hivi huwezi jua hata next move ni nini, ila options ni chache tu.

1. Lissu hawezi shinda uenyekiti. Zile technic zinazotumiwaga na Chama kubwa za wajumbe kutekwa, kufungiwa hotelini, wale wanywe huku simu zao zimekusanywa sasa ndio tegemeo pekee la team Mboowe. Na hii itafanya kazi. Njaa ni mbaya sana, hao wajumbe wengi ni njaa.

2. Uchaguzi ukiisha Chadema hapatakuwa kunakalika tena, Lissu atahamia Chama kingine au ataanzisha chama chake, na kitapata uungwaji mkono ndani na nje ya nchi.

3. Lissu is upto 2025 presidential election, kitu ambacho kina Mboowe hawataki, wanataka mtu laini laini kwa uchaguzi wa 2025, CCM ipite kwa changamoto nafuu, kwa hili Lissu ashajiandaa kugombea kupitia chama kingine/kipya.

Baada ya 2025 nguvu ya ACT itakuwa juu ya Chadema. Atleast ACT itaokoteza wabunge wengi Zanzibar, Chadema haitofikisha majimbo 8 bara. Mvuto utakuwa umepotea kabisa.
 
Kuanzisha chama sio jambo rahisi hapa Tanzania inakuchukua zaidi ya mwaka, lazima ukwamishwe na chama tawala kilicho nyuma ya Mbowe.
 
Sio rahisi kihivyo, zitto chama chake kina majimbo mangapi?
 
Sio rahisi kihivyo, zitto chama chake kina majimbo mangapi?
Huwezi judge idadi ya wabunge kwa 2020 rigged election, ule ulikuwa uchafuzi na sio uchaguzi. Well, Chadema ilipata Mbunge Mmoja (ilimtenga ofcourse), na Covid 19 (hawa waliingia Bungeni kwa signature ya Mnyikq na baraka za Mwenyekiti).
 
Kuanzisha chama sio jambo rahisi hapa Tanzania inakuchukua zaidi ya mwaka, lazima ukwamishwe na chama tawala kilicho nyuma ya Mbowe.
Ndio maana ana option ya kuamia chama kingine. Possibly ACT.
 
2015 Mbowe amekula hela ya Lowassa.
2020 Mbowe amekula hela ya Magufuli.
2025 Mbowe anataka kula hela ya Samia.

Huyu muhuni anapenda hela kuliko siasa na chama.
 
Chadema haitofikisha majimbo 8 bara. Mvuto utakuwa umepotea kabisa.
Kitendo cha Mbowe kuchukuwa fomu ya kugombea uenyekiti tu, imepoteza 50% ya uungwaji mkono.

Mbowe akishinda 45% ya uungwaji mkono inaenda kuanguka. Hivyo itabakia na 5% tu ambayo kwa %kubwa ni machawa.
 
Lisu anagombea kupitia ACT, Lisu na Zito wanaiva na wataungana kumkomuadabisha Mbowe 2025, Revange is real
 
Sio kweli aliokuwa hajajipanga kugombea mwenyekiti ni baada ya kuona wenje ametangaza nia ya kuwania umakamu ndipo alipo badili uwelekeo wake kwasababu alijua anaenda kupigwa chini
 
Sio kweli aliokuwa hajajipanga kugombea mwenyekiti ni baada ya kuona wenje ametangaza nia ya kuwania umakamu ndipo alipo badili uwelekeo wake kwasababu alijua anaenda kupigwa chini
Trend inaonyesha alijua mapema, na ili kina Mbowe wasijipange mapema, akiwa airport aliulizwa utagombea uenyekiti, akajibu hapana, body language yake ikionyesha kuna ukakasi kwenye jibu lake. Pia kusema anataka tetea umakamu ilikuwa ni poteza boya tu, angalia kina Lema na Heche walivyojiweka mbali na chama kwa muda mrefu, yote hayo walishayajadili kabla, kwenye siasa hakuna cha bahati mbaya, kila kitu ni mipango.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…