Uchaguzi 2020 Lissu: Ili uchaguzi uwe huru na haki ni lazima mawakala wote waapishwe

Uchaguzi 2020 Lissu: Ili uchaguzi uwe huru na haki ni lazima mawakala wote waapishwe

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu amesema ili uchaguzi uwe huru na haki ni lazima mawakala wote waapishwe.

Amesema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni Mombo, amesema Sheria ya Tume ya Uchaguzi inasema mawakala wanaweza kuapishwa hata kwenye ofisi ya kata.

Sheria hiyo imekuwa kinyume kwa kuwa Tume imewataka mawakala wakaapishwe kwenye ofisi ya Mkurugenzi.

Aidha amesema amesikia Mkurugenzi wa Chato amekataa kuapisha mawakala wa CHADEMA kwa kuwa barua zimefojiwa, amehoji ni tangu lini mkurugenzi anakuwa mtaalamu wa miandiko
 
Safi sana. Tukiwa wapole katika hili,tumeliwa.Ni bora kupambana, iwe mvua, iwe jua; vinginevyo, uchaguzi wote utakuwa hauna maana na wapendaa mabadiliko tutakuwa tumeshindwa kabla hata kura hazijaanza kupigwa.
 
Sijasoma ili gazeti lakini ninachoweza kusema ni kwamba, Magufuli anadeserve mitano tena.. ndugu zangu tulichelewa ..
 
Watu wanaandikiana barua za kuomba mamilion wewe unahangaika na vibarua vya mawala, umasikini wa akili, tafuta sababu nyingine siyo hiyo we mkutugenzi uchwara
 
Nenda wewe kwenye huoumilionea maskini kama mm acha dharau
Watu wanaandikiana barua za kuomba mamilion wewe unahangaika na vibarua vya mawala, umasikini wa akili, tafuta sababu nyingine siyo hiyo we mkutugenzi uchwara
 
Back
Top Bottom