Uchaguzi 2020 Lissu, je wananchi wa vijijini watazitumia hizo reli unazotaka kuzijenga Dar?

Nakubaliana na wewe kuwa maendeleo ya vitu yaendane na mahitaji ya watu kwa maendeleo yao.

Sikubaliani na wewe ya hiyo mifano uliyotoa kwa kuwa yanakisi mtazamo wako kisiasa zaidi kuliko kiuchumi/maendeleo.

Miradi yote iliyotekelezwa au inaendelea kutekelezwa na Serikali iko kwenye Ilani ya Uchaguzi Mkuu, 2015 ya CCM. Ni Ilani iliyokipa chama ridhaa ya kuunda Serikali. Ni imani kuwa Ilani hiyo, ilivyoboreshwa kwenye Ilani ya Uchaguxi Mkuu, 2020 itakipa CCM ushindi mnono ukilinganisha na Ilani ya CHADEMA ya Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu.
 
Mnaongelea maendeleo ya watu kinadharia tu. Km hali ya mkulima kimapato itabadilika bila kuwa na soko? Je, soko ni majirani zake tu? Hivyo basi, huyu mkulima aondokane na umaskini wa kipato lazima kuwepo na miundombinu imara na bora ya hifadhi ya mazao na usafirishaji (reli, barabara, majini na angani) mazao yaweze kuwafikia walaji kwa wakati na ubora uleule.
 

..tatizo la ccm ni kupotosha.

..sasa wewe ni victim wa upotoshaji wa ccm.

..miundombinu anayoipinga TL ni ile ambayo ina harufu ya ufisadi, na isiyowagusa wananchi.

..kwa mfano, airport ya Chato, wananchi wa Chato waliulizwa kama wanahitaji uwanja wa ndege wakasema hapana.

..lingine ni ununuzi wa ndege na kuifufua atcl. Ukweli ni kwamba mradi huo ni wa hasara. Pia tayari kulikuwa na mashirika ya ndege yanayoleta watalii toka nje, na mengine yanayosafirisha abiria wa ndani.

..Trillions of shillings zilizotumika kununua ndege na nyingine kuingia ktk mifuko ya wakubwa zingeweza kuanzisha miradi inayogusa wananchi wengi zaidi hapa nchini.

..Again, lazima kuwe na balance kati ya maendeleo ya vitu na maendeleo ya watu. Maendeleo ya vitu lazima yawalenge na yawanufaishe WATU.
 
Mpo vijana mbona hampendi kufikirisha hizo akili kila saa mnawaza mgando tu

Sent from my BLL-L22 using JamiiForums mobile app
 
Hii Awamu ya Tano imeleta watu wajinga kila mahali mpaka wasomi wenye akili na uwezo hawaeleweki na wanapoleta maoni yao yenye tija wanachukuliwa na vilaza wasaka teuzi kama huyu kuwa ni wapinga Miradi ya viongozi walio madarakani. Tundu Lissu ana akili, ujuzi na uwezo kuliko wagombea wote wa Urais na anachosema kuhusu usafiri Dar ni kweli kabisa kunahitajika mwingine zaidi ya Mabasi ya Mwendo Kasi ambayo ni Mabasi ya kawaida tu. Mabasi haya yanaitwa ya Kasi kwa sababu yanapita kwenye barabara ambako vyombo vingine vya usafiri haviruhusiwi kupita. Waliobuni Mradi wa Mabasi hayo walikuwa na akili kama za Lissu ambazo kwa bahati mbaya viongozi wa sasa, ikiwa labda ni pamoja na wasimamizi wa Mradi, hawana na wanapongezana kwa ufanisi. Hizo barabara za hayo Mabasi zilipanuliwa sana ili Mabasi ya kwenda upande mmoja yaende bila bugdha na yale ya upande wa pili nayo vivyo hivyo yaende bila shida na katikati ya njia mbili za Mabasi ilianchwa nafasi pana sana njia nzima wavuka kwa miguu wana madaraja yao ili wasigongwe. Sisi wa bara tunashangaa kuwa vilaza wanaachwa wawasemee viongozi wetu wote wa nchi hii walioko Dar mpaka waonekane hawajui kwa nini hizo barabara za Mabasi Kasi ni pana hivyo na wakazi wa Jiji hawaruhusiwi kutumia maeneo ambayo Mabasi hayapiti. Nafasi katikati ya barabara za Mabasi ilianchwa ili wakati ukifika na fedha ikipatikana zijengwe reli za treni (trams) mbili moja ya kwenda upande mmoja na ya pili upande wa pili bila kukutana. Baada ya barabara ya kwanza ya mabasi kufunguliwa mkandarasi wa reli angeanza kutandika reli na mpaka leo labda line moja ingekuwa imekamilika tayari kuanza kutumika. Treni hizo ndizo Lissu anazungumzia na zitakuwa zinapakia watu wengi zaidi kuliko Mabasi kwa gharama ndogo za uendeshaji maana zitatumia umeme na zitapita kwenye njia zao bila kuingiliwa na vyombo vingine vya usafiri. Wengi wa Dar wanakumbuka zile treni za Mwakyembe ambazo zilikuwa za TRC za safari ndefu na uzito mkubwa kwa hiyo gharama kubwa za uendeshaji
 
Reactions: BAK
Selikari za majimbo kila Jimbo litaamua kushughulika na priorities,

Jimbo la dar litakenga brbr na reli Kama njia ya kurahisisha usafiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…