Haya ndugu zangu
Lissu anaendelea kupitisha dozi huko. Hii statement alivyoitoa mahakamani kila mtu alicheka
============
Mhe. Lissu: Kwenye ushahidi wako jana, ulisema nilihojiwa na mtu mmoja na mwingine alichangia kwa kuniuliza maswali mbalimbali, waeleze majaji kama hayo maneno yapo katika maelezo yako?
Shahidi wa kificho P9 : Hayapo.
Mhe. Lissu: Niliona clip ya Tundu Lissu ndio nikaanza, waeleze hayo maneno kama yapo katika maelezo yako.
Shahidi wa kificho P9 : hayapo.
Mhe. Lissu: Sijamalizana na wewe, nataka ukitoka hapa ukawaeleze Mapolisi kwamba kule hakufai!
Watu wanacheka: ππππ
Mhe. Lissu: Ulisema mimi kama mwananchama wa CHADEMA nilishawishika na kwamba nitafanya uasi, hayo maneno yapo au hayapo?
Shahidi wa kificho P9: Yapo.
Mhe. Lissu: Sasa nataka uwaambie majaji kwamba wewe ni Mwanachama wa CHADEMA au sio?
Shahidi wa kificho P9 : Mimi sio mwanachama wa CHADEMA.
NB: Mahakama Ilikataza kesi kwenda live kupitia vyombo vya habari na ndio maana hakuna video wala audio