Uchaguzi 2020 Lissu: Msichague viongozi wasaka fedha

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mgombea urais kupitia Chadema, Tundu Lissu amewataka Watanzania kuchagua viongozi ambao hawatakwenda kwenye mabaraza ya madiwani na bungeni kusaka fedha.

Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti wa Chadema ameeleza hayo leo Jumatatu Oktoba 26, 2020 katika mkutano wa kampeni jimbo la Handeni mkoani Tanga.

Uchaguzi mkuu wa Tanzania unafanyika Jumatano Oktoba 28, 2020 siku ambayo Lissu amewataka wananchi kutofanya makosa kwani uchaguzi ni mustakabali wa maisha yao.

Amesema baadhi ya wagombea hawafikirii kutetea maslahi ya waliowachagua wala kuihoji Serikali kwenye vyombo hivyo, bali wanaangalia namna ya kupata fedha.

“Hakikisheni Oktoba 28 hamuendi kufanya makosa kwa kuchagua viongozi wanaokwenda kutetea maslahi yao, awe kiongozi anayefikiria kuhusu wale waliomchagua msipofanya hivyo mnaweza kujutia,” amesema Lissu.

Alitumia mkutano huo kuwaahidi wakazi wa Handeni kwamba akiwa rais atafuatilia na kutafuta ufumbuzi wa mgodi wa Magambazi ili uendelee na kazi.
 
Haiwezekani kabisa huyo kibaraka wako kushinda, akifikisha asilimia moja atakuwa na bahati. Acheni ubwege wa kujipa matumaini hewa

Bora uchaguzi uishe arudi zake Belgium...
Kwani wanatarajia kumpiga risasi nyingine ili.aende kutibiwa Ubelgiji au ubelgiji arudi kwa ajili gani?

Tundu Lissu ameishi Ubelgiji sio kwa amri yake ila ni katika harakati za kupigania uhai, wake.

Akiwa Waziri wakati wa Mkapa Magufuli aliwahi kukaa ujerumani kwa matibabu baada ya kuugua ghafla.

Kwahiyo kutibiwa kunaweza kukufanya uwe mahali popote katika harakati za kupigania uhai wako
Haiwezekani kabisa huyo kibaraka wako kushinda, akifikisha asilimia moja atakuwa na bahati. Acheni ubwege wa kujipa matumaini hewa.

Haiwezekani kabisa huyo kibaraka wako kushinda, akifikisha asilimia moja atakuwa na bahati. Acheni ubwege wa kujipa matumaini hewa.
VIBARAKA WAKO KATIKA NAMNA TOFAUTI NCHI HII

Ukitaka kujua beberu halisi hapa nchini fikiria hivi.

Tanzania ni nchi masikini,hilo halina ubishi na Tanzania inategemea kilimo na wananchi wake 70% wanategemea kilimo.

Marekani na Canada ni mataifa tajiri sana Duniani na ndio huko kuna watu tunao waita mabeberu.

Sasa twende kwenye hoja, hivi kiongozi wa nchi kama Tanzania, unaweza kutumia busara gani, kuwakopa wakulima masikini mazao yao, halafu ukawa na ujasiri wa kutumia hela hiyo hiyo uliyo paswa kuwalipa wakulima na kwenda kuwalipa CASH matajiri mabeberu wa Marekani na Canada, ili wakuuzie ndege ambazo zinatumiwa na 2% ya watanzania wote!?

Tukisema viongozi wanao fanya maamuzi hayo wanakua na maslahi binafsi na wanakua ni sawa na mawakala wa mabeberu tunakua tumekosea!?

Halafu wanasema yeye ni wa wanyonge,wanyonge wapi !?
 
Mbowe na genge lake ndio wasaka pesa namba moja. Baada ya kukusanya michango ya kutosha kwenye kampeni ndio analeta dharau kwa mashabiki zake. Saccos out
 
Duh! Hatuwezi kulifafanua vizuri zaidi yako🤝
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…