Lissu na Gen Z humuwezi kutumia mbinu za mwaka 47 na kutegemea kufanikiwa wakati huu wa kidigitali, nyumbulikeni!

Lissu na Gen Z humuwezi kutumia mbinu za mwaka 47 na kutegemea kufanikiwa wakati huu wa kidigitali, nyumbulikeni!

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Sasa tunashuhudia mwamko mkubwa hasa upande wa vijana kwenye masuala ya siasa na uchaguzi, japokuwa uchawa umetaradadi kwa kiasi kikubwa, kuna mwanga umeanza kuonekana na kuashiria huenda jua likaangaza baada ya kuwa kwenye kiza kwa muda mrefu.

Wakati hayo yote yanatokea hatuwezi kukataa kuwa zama zimebadilika, watu na tabia pia zimebadilika. Huwezi ukatumia mbinu zile zile za mwaka 47 na kutegemea kupata matokeo makubwa wakati huu ambako mambo yamesogea sana.

Toka miaka ile ya nyerere mobilization zilikuwa zinafanyika ana kwa ana, watu wanajizoa na kwenda barabarani, polisi wanakuwa wanajua mambo yenu yoteee, yaani mko predictable, wana mikeka yote ya jinsi ya kuwadhibiti. Sasa unakuja kutumia mbinu hizi hizi tena wakati huu ambako mambo yameendelea na hata hawa jamaa wamebadilisha mbinu lakini nyie bado mnataka mbaki kule kule.

Kuna wakati CHADEMA mlifanya maandamano afu mkaacha polisi waandamane, that was good.. lakini ikaishia hapo, sijui aliyepanga mchongo alihamia CCM😂😂.

Sisemi msijifunze kutokana na historia, hapana. Ya nyuma yawape mwongozo ya kupambana ki sasa. Maandamano yanaweza kuendelea lakini mobilization ikabadilika ikaanzia mtandaoni mkija kulianzisha mtaani inakuwa ni kuhitimisha, hapo kuwanakuwa hakuna kurudi nyuma.

Walimu wa NETO mngeweza kujimobilize zaidi, mpaka mnakuja kufanya mkutano walimu wote ambao hawana ajira nchi wangekuwa nyuma yenu, kiongozi ameshikwa jumuia za mikoa yote ya walimu zinasimama, yaani ubaya ubwele. Mpaka CCM/Serikali inakuna kichwa. Lakini sasa kiongozi kashikwa hata walimu wenyewe ambao hawana ajira wako kimya! Ukute hata ni robo tu ndio walikuwa na taarifa hiyo.

Teknolojia siyo kwaajili ya kufanyia biashara tu hata mapinduzi yanaweza kufanyikia huko. CCM wanaenda kasi zaidi na kupush hastags, kusambaza taarifa fakes na AI, wana mifumo thabiti ya kutrack wanachama wao na kuwafikia popote walipo, yaani wamejipanga.

CHADEMA hamuwezi kosa watu wa kuwasaidia kwenye sehemu huu, vijana halkadhilika, mmezaliwa kipindi hiki ambako unakua na kuingia moja kwa moja kwa teknolojia, yaani mambo yako damuni, kizazi cha dot.com, sasa na nyie mnarudije nyuma tena kuanza kutumia mbinu za miaka 47 kushindana na kundi ambalo linajitahidi kwenda na wakati kuwaangamiza?

Amkeni mbadilishe TZ iwe kama New Yoki... nyumbulikeni!
 
Back
Top Bottom