Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Mgombea nafasi ya mwenyekiti wa CHADEMA ndugu Tundu Lissu, jana katika mdahalo uliorushwa na Star TV ukiongozwa na mwandishi wa habari Chief Odemba. Alisema kuwa anaikubali dhambi ya kushiriki kumfanya Lowassa kuwa mgombea wa CHADEMA mwaka 2015.
Maneno hayo yalitokana na swali aliloulizwa na Nyanda kuwa, CHADEMA ilimuita Lowassa fisadi kwa miaka saba, lakini cha ajabu chama hicho kikamfanya kuwa mgombea wa urais wa chama hicho na Tundu Lissu akiwa mshiriki mkubwa ndani ya chama katika kufanya hilo.
Lissu akajitetea kuwa dhambi hiyo yeye anakubali kuibeba, ila akaendelea kujitetea kuwa Kiukweli kabisa yeye na Mnyika walikuwa ni watu wasiomkubali Lowassa kabisa isipokuwa Walifichwa kuhusu Ujio wake mpaka dakika ya mwisho kabisa ya Ujio wake.
Walikuja kuambiwa kuwa Lowassa anaingia CHADEMA kuwa mgombea siku moja kabla ya mkutano wa kamati kuu. Na kwenye mkutano wa kamati kuu Majority ya Wajumbe waliunga mkono Lowassa kuingia CHADEMA na kuwa mgombea. Akasema na yeye akaamua kwenda na wengi. Hata hivyo amekiri dhambi hiyo.