Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Kweli siasa ni sayansi, anachokifanya Lissu ni sayansi ya siasa, inahitaji akili zaidi kuliko nguvu, pesa au ujanja ujanja.
Nani anaweza kuamini kuwa leo hii Mbowe tayari yuko nje wa mkondo wa siasa za upinzani? Yote hayo ni matokeo ya harakati za Tundu Lissu katika kuwania uenyekiti wa Chadema.
Leo hii Mbowe hajui tena hatma yake ya kisiasa ndani ya Chadema na nje ya Chadema. Anaonekana mwenye msongo mkubwa wa mawazo, hajiamini, amechoka, anaongea majuto, analalamika, amefadhaika na kufedheheka, kisa tu uchaguzi wa ndani ya Chadema.
Makamanda wengi wa Chadema kwa sasa wanamuona Mbowe kama Mrema, Lipumba au Cheyo aliyechangamka. Leo hii CCM na serikali yake wanamshangilia Mbowe, wanamkumbatia Mbowe, wanampigia kampeni, wanamfadhili, wapo tayari kumpigania ashinde kwa heri au shari. Kisa Lissu, Lissu, Lissu!