Uchaguzi 2020 Lissu nichagueni ili nitengeneze mfumo mpya wa kiongozi kupitia katiba mpya

mcoloo

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
918
Reaction score
1,402
Tundu Antipas Lissu, amekuwa alisisitiza kuwa Kama watanzania watakuwa na Nia ya kupata katiba mpya, Basi 28/10/2020 atakaye mpigia kura atambue kuwa kura yake itakuwa Ni kura ya katiba mpya.

Hili Ni Jambo lisilo stahili kupuuzwa hata kidogo, Mara tu baada ya serikali hii ya awamu ya tano kuingia madarakani taasisi mbali mbali na makindi mbali mbali ya kijamii vili muomba Rais Magufuli arejelee mchakato wa katiba mpya , ili tuweze angalau kuwa na katiba inayo endana na mfumo wa vyama vingi vya siasa. Matokeo yake Rais alisema kuwa hakuwahi kuzungumzia habari ya katiba mpya na jinsi ilivyo hata Leo kwenye kampeni zake hataki kabisa kuligusia Hilo.

Na anafanya hivyo kwa makusudi
1: Anatambua kuwa Kama akikubali Itawanyang'anya mamlaka mengi ya kiutendaji aliyojimiliksha kutokana mfumo uliopo kwa sasa.

2: Anatambua kuwa Kama ataruhusu huo mfumo mpya wa katiba utaweza kuwa kichochezi Cha wao kutoka madarakani kiurahisi kwani utaweza kuruhusu kuhoji uhalali wa matokeo ya uchaguzi mahakamani ( Kama ingeonyesha kuna mchezo mchafu )n.k.

Hivyo Tundu Lissu anatoa wito kuwa Kama kweli tuna Nia na katiba mpya itakayo ondolea mbali mfumo wa viongozi kung'ang'ania kwenye madaraka hata Kama wananchi wamewachoka basi 28/10/ 2020 tutambue kuwa kura yako itakuwa Ni kwa ajili ya katiba mpya.
Ukweli Ni kwamba katiba mpya inahitajika. Uamuzi Ni wako na wangu.
 
Tunahitaji katiba mpya la sivyo nchi hii haiwezi kuendelea.
 
Naona kila mwana CCM analikwepa suala la FAO LA kujitoa kama vile ni Jambo dogo. Bwana Humprey Polepole ameongea na waandishi wa habari Mara 2..hii hoja ameiruka.

Mtu amefukuzwa kazi au mkataba umeisha, NSSF (Fao la kukosa Ajira) wanasema ulipwe 33.3 % ya Mshahara kwa miezi 6...baada ya hapo kaa miezi 18 ...ndio ulipwe.

Sheria mpya ya 2018, Raisi Magufuli alisaini, lakini baadae akaja kufuta kikokotoo cha wastaafu pekee...Sasa wafanyakazi wanaofukuzwa kazi sekta binafsi kabla ya umri wa kustaafu wanataabika. Wenye kuona hili wamshauri Magufuli haraka sana na arekebishe maana Katiba imempa mamlaka.

Raisi Magufuli, rudisha FAO LA kujitoaa. watu walipwe pesa zao kwa mkupuo bila masharti ... Hiki ni kipindi cha Kampeni...Kura za Wafanyakazi sekta binafsi ni mamilioni...

Ndugu Bashiru na Pole pole...FAO LA Kujitoa..
 
... awamu hii imeonesha umuhimu wa Katiba Mpya; imeonesha ni kwa jinsi gani akija mtawala mshenzi anaweza kuitumia Katiba hii hii iliyopo kuwa dikteta kamili kama alivyowahi kusema Mwl. Nyerere kwamba Katiba hii inampa uwezo huo kama angetaka ila bahati nzuri yeye na waliomfuatia walikuwa na hofu ya Mungu kwa kiwango chao hawakutaka kwenda huko.

... ila kwa hakika akija "mpuuzi" tumekwisha; sio CCM, wala Chadema, wala ACT, taifa zima litaisoma namba. Katiba Mpya itakayo-regulate madaraka ya mihimili na viongozi ni muhimu sana kwa faida ya taifa zima.
 
Hahaha kwani huyo mtawala mshenzi hajaja?!
 
Wata
Tundu Antipas Lissu, amekuwa alisisitiza kuwa Kama watanzania watakuwa na Nia ya kupata katiba mpya, Basi 28/10/2020 atakaye mpigia kura atambue kuwa kura yake itakuwa Ni kura ya katiba mpya.

Hili Ni Jambo lisilo stahili kupuuzwa hata kidogo, Mara tu baada ya serikali hii ya awamu ya tano kuingia madarakani taasisi mbali mbali na makindi mbali mbali ya kijamii vili muomba Rais Magufuli arejelee mchakato wa katiba mpya , ili tuweze angalau kuwa na katiba inayo endana na mfumo wa vyama vingi vya siasa. Matokeo yake Rais alisema kuwa hakuwahi kuzungumzia habari ya katiba mpya na jinsi ilivyo hata Leo kwenye kampeni zake hataki kabisa kuligusia Hilo.

Na anafanya hivyo kwa makusudi
1: Anatambua kuwa Kama akikubali
Itawanyang'anya mamlaka mengi
ya kiutendaji aliyojimiliksha
kutokana mfumo uliopo kwa sasa.
2: Anatambua kuwa Kama ataruhusu
huo mfumo mpya wa katiba
utaweza kuwa kichochezi Cha wao
kutoka madarakani kiurahisi kwani
utaweza kuruhusu kuhoji uhalali
Wa matokeo ya uchaguzi
mahakamani ( Kama ingeonyesha
kuna mchezo mchafu )n.k.

Hivyo Tundu Lissu anatoa wito kuwa Kama kweli tuna Nia na katiba mpya itakayo ondolea mbali mfumo wa viongozi kung'ang'ania kwenye madaraka hata Kama wananchi wamewachoka basi 28/10/ 2020 tutambue kuwa kura yako itakuwa Ni kwa ajili ya katiba mpya.
Ukweli Ni kwamba katiba mpya inahitajika. Uamuzi Ni wako na wangu.
Watanzania Wote kwa pamoja tunahitaji Katiba Mpya ! Kipaumbele chetu kwa sasa ni kupata Katiba mpya . Watanzania Wote bila kujali tofauti zao za Kiitikadi za Vyama , Wanahitaji Katiba Mpya .
 
Back
Top Bottom